Habari za Punde

Rais Kikwete aagana na Mabalozi Wapya Ikulu Dar-es-Salaam.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mabalozi saba walioteuliwa hivi karibuni na kuagana nao kabla hawajaripoti kwenye vituo vyao katika nchi mbali mbali leo Ikulu jijini Dar es salaam. Mabalozi hao toka kushoto ni Mhe Modest Melo anayekwenda Umoja wa Mataifa, The Hague, Geneva, Mhe Mabrouk n. Mabrouk (Abu Dhabi – Umoja wa Falme za Kiarabu – UAE), Luteni Jenerali Mstaafu Abdulrahman Shimbo (Beijing, China), Mhe Anthony Cheche (Kinshasa - Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC), Mhe Chabaka Kilumanga (Visiwa vya Comoro), Mhe Wilson Masilingi (The Hague, Uholanzi) na Mhe Liberata Mulamula (Washington DC, Marekani).  PICHA NA IKULU

2 comments:

  1. Tunashanga sana mabalozi karibu10 mzanzibar mmoja,tuksema huu simuungano ni ukoloni wa kitanganyika. ngojeni siku na miaka inakaribia, chakachuweni daftari, lakini mjue wazanzibar tuta wa chagua Cuf, muamsho mtakiono 2015

    ReplyDelete
  2. Anony 1.. Manenoyako mazima kabisa, kwakuongezea tu.

    Na huyo mmoja aliepelekwa atakua ni Muhafidhuna kama Mzale, na Ali Karume. Na hiyo nchialiopelekwa ni UAE..

    Kwanini Wasiwe Wabunge eatlist 4 kutoka Zanzibar na 6 kutoka Tanganyika...Mabalozi wote katika Nchi Muhimu sana ambazo zinaweza kuleta maendeleo na usiano wa Nchi zetu huwa wanatoka Tanganyika. Wazanzibari tushaambiwa hatuna Elimu ya kuwa Mabalozi.. Na ukiwatizama hao wenye elimu ni hao Waliohushi Vyeti nakujichukulia PHd za Ulaya mara 4x4..

    Phd ya Ulaya hata mimi naweza kuichukua kwani unapewa kazi na tools zote zakuandika Thesies. Na unapata advices kutoka mwanzo mpaka mwisho. Sasa hakuna atakaeweza kufeli .

    Hakuna lenye mwanzo lisiokua na mwisho. Inshallah Allah atatupa tulitakalo na Nchi yetu itakua huru Amin.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.