Habari za Punde

Dk Shein ahudhuria Sala ya Idd leo

IMG_3014 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj Dk.Amani Abeid karume wakati wa Swala ya Idd el Fitri iliyosaliwa Kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman,Mjini Unguja.[Picha na Ramadhan  Othman Ikulu.]
IMG_3028 Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji ,akiswalisha Swala ya Idd el Fitri,ambayo kitaifa iliwaliwa leo katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja leo katika kufuatia kumalizika kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3038 Baadhi ya wananchi na waumini wa Dini ya Kiislamu wakiwa katika swala ya Idd el Fitri,iliyoswaliwaa kitaifa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3042 Akina mama waumini wa Dini ya Kiislamu wakiswali swala ya Idd el Fitri katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja,kufuatia kumalizika kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3055 Imamu Mkuu wa Msikiti Masjid  Mushawal Mwembeshauri Sheikh Mziwanda Ng’wali Ahmed,akitoa hutuba ya swala ya idd el fitri,katika viwanja vya maisara Suleiman Mjini Ungujaleo katika kusherehekea sikukuu hiyo kwa wailamu wote Duniani.

[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

2 comments:

  1. Nimefurahishwa na uamuzi wa kuirudisha Sala ya Idd viwanjani kuhuisha Sunna ya Mtume Rehma na amani juu yake.

    Ninawapa mkono wa idd na pia shukurani kwa wale wote walioweza kutoa ushauri huu wa kuiondoa Sala hii msikitini na kurudishwa kiwanjani kama ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo Sala hii ilikuwa ikisaliwa katika Viwanja vya Kisiwandui ilipokuwa afisi kuu ya ASP

    Mpaka pale ambapo Mashekhe wa wakati huo walipoingizwa katika mtihani ambao mpaka hii leo bado Mashekhe wetu wameshindwa au kukosa ujasiri wa kuwashauri vizuri hasa Serikali na masuala ya uwekaji masanamu kwa mujibu wa taratibu za dini yetu ya kiislamu

    ReplyDelete
  2. Nashukura kwa kutupatia habari na picha za Sala ya IDD iliyofanyika huko nyumbani. But sala hiyo ya IDD si kwa waislamu wote Ulimwenguni kwani Nchi za Kiarabu ukiitoa Oman wamesheherekea na kusali sala ya IDD tokea siku ya Alhamis tarehe 8.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.