Habari za Punde

Kampeni dhidi ya udhalilishaji watoto yazinduliwa Chakechake, Pemba


WANANCHI mbali mbali na wanafunzi wa skuli za sekondari kisiwani Pemba, wakifuatia kwa makini mchezo wa kuigiza, kutoka katika kikundi cha Sanaa Gombani Pemba, juu ya uzinduzi wa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, Inayojulikana kama ni “Daladala yangu ni salama kwa watoto” huko katika steni ya dalalala chake chake (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

WANAKIKUNDI cha Sanaa kilichopo gombani Pemba, wakiigiza moja ya maigizo igizo, katika uzinduzi wa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, Inayojulikana kama ni “Daladala yangu ni salama kwa watoto” na kuwafanya madereva wa gari za abiria kuacha kazi zao na kuangalia igizo hilo kama wanavoonekana katika picha, huko katika steni ya dalalala chake chake (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

VIONGOZI mbali mbali wa Serikali, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wanawake na Watoto Zanzibar Rahma Ali Khamis wapili kutoka kushoto, katika hafla ya uzindizi wa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, inayojulikana kama “Daladala yangu ni Salama kwa watoto’ huko katika steni ya daladala chake chake. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

AFISA Tawala wilaya ya Chake Chake, Rashid Khadid akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Mwanajuma Majid Abdalla katika hafla ya uzinduzi wa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, inayojulikana kama “Daladala yangu ni Salama kwa watoto” huko katika steni ya daladala chake chake. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

AFISA Tawala wilaya ya Chake Chake, Rashid Khadid akibandika Stika katika daladala ya Chake-Wete, kuashiria uzinduzi wa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, inayojulikana kama “Daladala yangu ni Salama kwa watoto” kama anavyoonekana katika picha, huko katika steni ya daladala chake chake. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MKURUGENZI wa Wanawake na Watoto Zanzibar, Rahma Ali Khamis akibandika stika katika daladala ya Chake-Wete, mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, inayojulikana kama “Daladala yangu ni Salama kwa watoto” kama anavyoonekana katika picha, huko katika steni ya daladala chake chake. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

MKUU wa askari wa usalama wa barabarani Mkoa wa kusini Pemba, Shawal Abdalla akibandika stika katika daladala mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, inayojulikana kama “Daladala yangu ni Salama kwa watoto” kama anavyoonekana katika picha, huko katika steni ya daladala chake chake. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

WANANCHI wakibandika stika katika daladala mbali mbali zilizokuwepo steni, mara baada ya kuzinduliwa kwa kampeni dhidi ya udhalilishaji wa watoto, inayojulikana kama “Daladala yangu ni Salama kwa watoto” kama anavyoonekana katika picha, huko katika steni ya daladala chake chake. (Picha na Abdi Suleiman, Pemba.)

1 comment:

  1. Hayo mashaka mengine tunaletewa. Wenzetu wa magharibi kila linalowashinda wao huko then wanatuletea sisi. Uzazi wa mpango, watoto kupewa uhuru kupita kiasi, haki za wanawake. Tuache kuuza dini na utu wetu kwa matumbo yetu tusiwe tunabeba kila kitu tunachiletewa kuna mtoto gani anaedhalilishwa kwa Unguja na Pemba? haya tusubiri nasie mtoto wako wa miaka 12 akuletee boy friend nyumbani

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.