Kampuni
ya simu za mkononi ya Zantel, leo imetangaza kudhamini semina za kuhamasisha
vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini zitazoendeshwa kwenye zaidi ya mikoa
13 kwa kushirikiana na Clouds Media Group.
Semina
hizo ambazo zinaenda sambamba na ziara ya kimuziki ya tamasha la Fiesta ambalo
mwaka huu litaenda zaidi ya mikoa 13, zinatarajiwa kufanyika siku moja kabla ya
tamasha kila mkoa ambao Fiesta inaenda.
Mada
zitakazojadiliwa kwenye semina hizo ni pamoja na ubunifu, ujasiriamali,
Uongezaji thamani kwenye bidhaa au shughuli yoyote unayofanya pamoja na kujenga
ushirikiano, uwekezaji pamoja na lugha.
Akizungumzia
semina hizo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, amesema kampuni yake
imekuwa msitari wa mbele katika kuwawezesha vijana, na kwa semina hizi wanaamini
vijana wengi watapata nafasi ya kuzitambua na kujifunza.
‘Tanzania
ina fursa nyingi sana kwa vijana, na sisi Zantel tunaamini nafasi hii itakuwa
muhimu kwa vijana kujifunza na kutambua fursa zilizopo kutoka kwa wataalamu
mbalimbali’ alisema Khan.
Naye
Mkurugenzi wa Utafiti na Uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba,
alisema nchi ya Tanzania ina fursa nyingi lakini tatizo limekuwa ni namna ya
kuzitumia fursa hizo.
‘Tumeandaa
semina hizi kwa kutambua tatizo kubwa lilipo kwenye jamii yetu, umaskini na
ukosefu wa ajira kwa vijana, jambo ambalo semina hizi zitaenda kutatua’ alisema
Mutahaba.
Mojawapo
wa wazungumzaji kwenye semina hizo atakuwa Mrisho Mpoto, mwakilishi wa mfuko wa
hifadhi ya jamii (NSSF), Ruge Mutahaba pamoja na wageni waalikwa mbalimbali.
Kwa
mwaka huu semina hizo zimeanzia mkoa wa Kigoma, katika Ukumbi wa Kibo Hall
Park, na mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya.
No comments:
Post a Comment