Wasanii wa Kikundi cha Taarab cha Rahatul Dhamani kikitowa burudani katika sherehe hiyo kikiongozwa na Kiongozi wao Cholo Nganuni, wakiimbi wimbo wa Kisima, ulioimbwa na Kijukuu cha Siti Bint Saadi, katika ukumbi wa Salama Bwawani Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Hakimiliki Zanzibar Mtumwa Khatib Ameir, akitowa maelezo wakati
wa kukabidhi Tunzo na Mirabaha kwa Wasanii Zanzibar, waliojisajili katika Afisi ya Hakimiliki kuhusiana na kazi zao na kupatiwa malipo ya kazi hizo baada ya kutumika katika vituo mbalimbali vya TV na Redio, sherehe hiyo imefanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimsikiliza Afisa Mtendaji wa Hakimiliki Zanzibar Mtumwa Khatib Ameir, akitowa maelezo ya makabidhiano ya Mirabaha na Tunzo kwa Wasanii mbalimbali katika ukumbi wa Salama.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, akihutubia na kutowa Nasaha zake kwa Wasanii wa Zanzibar kujitokeza kusajili Kazi zao katika Afisi ya Hakimiliki Zanzibar kupata kipato kutokana na kazi zao sio kufaidika watu wengine kupitia kazi zao.
Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Abubakar Khamis Bakari, akizungumza wakati wa hafla hiyo katika ukumbi wa Salama bwawani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Afisi ya Hakimiliki Zanzibar Maryam Hamdan akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi Mirabaha Wasanii waliosajili kazi zao katika Afisi ya Hakimiliki Zanzibar jinsi watakavyofaidika na kazi zao baada ya kujisajili.
Wasanii wakifuatilia hutuba ya mgeni rasmin Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akihutubia katika hafla hiyo ukumbi wa Salama Bwawani.
Makamo wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimkabidhi Mwakilishi wa Kikundi
cha Taraab cha Malindi Fauzia Abdalla mrabaha(Fedha) baada ya kujisaji na kufaidika na kazi zao baada ya kutumiwa na vituo vya TV na Redio na maduka ya kurikodia nyimbo zao Zanzibar.
Mwakilishi wa Kikundi cha Taarab cha Culture Taimur, akipokea Mirabaha ya kikundi chao kutoka kwa Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, katika ukumbi wa Salama Bwawani.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, akimkabidhi Mirabaha ya Kikundi cha Taarab cha Spice Hassan Masoud, ikiwa ni malipo kwa kikundi hicho kutoka kwa Wadau wa Vyombo vya Matangazo Zanzibar kupitia TV na Rediokupiga nyimbo za kikundi hicho.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, akimkabidhi Mirabaha yake Msanii wa kizazi kipya Zanzibar Berry Black, baada ya kusajili kazi zake katika Afisi ya Hakimiliki Zanzibar na kupata faida ya kazi zake baada ya kujisaji. na kuwataka wasanii wazeke kujitokeza kujisali ili kupata matunda ya kazi zao wanazofanya.kupitia usanii wa muziki wa kizazi kipya na sanaa nyenginezo
Meneja Masoko wa Benki ya Watu wa Zanzibar Seif Suleiman, akimkabidhi Tunzo ya Utunzi na Ubunifu Msanii Haji Gora, wakati wa hafla ya kukabidhi Tunzo na Mirabaha Wasanii waliojisajili katika Afisi za Hakimiliki Zanzibar.Msanii Haji Gora Msanii wa Mashairi na mtunzi wa Vitabu ambavyo hufundishiwa maskulini Zanzibar na mtaalabu wa lugha ya Kiswahili na lahaja zake.
MENEJA wa Kampuni ya Simu ya Vodacom Zanzibar
Mohammed Mansoor Mohammed, akimkabidhi Tunzo ya Ubunifu wa Nembo Msanii Khamis
Faki, wakati wa hafla ya kukabidhiwa Wasanii Mirabaha yao na Afisi ya Hakimiliki Zanzibar
iliofanyika katika ukumbi wa Salama Bwawani
Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar Cable Mohammed Al Jabiry, akimkabidhi Tunzo ya Ubunifu Mwakilishi wa Msanii Marehemu Bi Kidude Bint Baraka kwa mchango wake katika ubunifu wa Sanaa ya Taraab na Unyango Zanzibar.
Berry Black akitowa burudani katika sherehe za kukabidhi Mirabaha (Fedha)Wasanii waliosajili Kazi zao katika Ofisi hiyo.
Waheshimiwa wameshindwa kustaamili katika viti vyao na kuinuka kumtunza Msanii wa Kizazi Kipya Berry Black akiimba wimbo wa kuhamasisha Wasanii kujisajili katika Afisi ya Hatimiliki kazi zao , wakati wa sherehe za kukabidhi Fedha Wasanii waliosajili Nyimbo zao katika Afisi ya Umuliki wa Hatimiliki Zanzibar zilizofanyika katika ukumbi wa Slama Bwawani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment