Habari za Punde

Vijana kuchangamkia fursa za mikopo ya elimu ya juu

Mstahiki Meya wa jiji la Zanzibar,  Mohamoud Muhamed Mussa amewataka Vijana  kuchangamkia fursa za mikopo ya elimu ya  juu ili kuwapunguzia mzigo wazazi wao.

Ameyasema hayo katika Ukumbi wa Baraza la Mji ,Michenzani Mall wakati wa Uzinduzi wa Program ya Uwezeshaji Vijana Kuendeleza Kielimu (Youths Educational Empowerment Loans).

Amesema kuwa kuzitumia fursa hizo za mikopo zinasaidia kurahisisha masuala ya elimu kwa vijana na kupunguka gharama  kwa wazee .

Aidha amesema wazee wamekuwa na jukumu kubwa la kulea kuendeleza pamoja na  kusomesha Vijana wao Kwa matumaini ya kuwa msaada wao wa baada hivyo  kinyume na hilo ni kupotea kwa maadili na malengo waliyoyatarajia.

Nae Mkurugenzi Muendeshaji wa Development Solutiom Gate (DSG) Ndugu  Waziri Gharib Khalid  amesema kuwa msingi wa Maendeleo ya Kijana hubebwa na mazingira Bora ya Uwezeshaji  Kitaaluma hivyo ni vyema Vijana Kujitokeza kwa wingi katika kujipatia fursa hiyo.

Amefahamisha kuwa Jumuiya  ya Development Solutiom Gate inaboresha mazingira ya elimu ili kuendana na Kasi ya Maendeleo nchini.

Jumuiya hivyo inatoa ufadhili kwa watoto Yatima  kuwaendeleza Kitaaluma na mikopo ya Kozi za muda mfupi yenye ufadhili wa asilimia mia zitazohusisha masomo ya Komputa na Lugha za Kigeni.



Imetolewa na Kitengo Cha Habari 
WHVUM.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.