Habari za Punde

Ibada ya Kuuombea Mwili wa Marehemu Sepetu Kanisa la Minara Miwili Zanzibar

Padri wa Kanisa la Minara miwili Shangani Cosmas Amani Shayo akiongoza Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu Isaac Abraham Sepetu, katika Ibada maalum ya kuuombea mwili huoiliofanyika katika kanisa hilo. 
Familia ya Marehemu Sepetu ikiwa katika Ibada ya kuuombea mwili wa Baba yao kabla ya kwenda kuzikwa kijiji kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja.
Msanii wa Luninga Wema Sepetu akiwa katika Ibada ya kuuombea mwili wa Baba yake katika Kanisa la Minara Miwili Unguja akiwa na mama yake na ndugu.
Wanandugu na Marafiki wakihidhuria mazishi ya Balozi Sepetu katika kanisa la Minara miwili wakati wa Ibada ya kuuombea mwili wa marehemu kanisani hapo. 
Padrin Cosmas Amani Shayo akiuombea mwili wa Balozi Sepetu wakati wa Ibada iliofanyika katika kanisa hilo.
Wasanii wa Luninga wakiwa nje ya Kanisa la Minara miwili wakihudhuria mazishi ya Baba wa msanii mwezao Wema Sepetu. 
Wananchi wakiwa nje ya Kanisa la minara miwili wakihudhulia mazishi ya Balozi Sepetu wakati ibada ya kuuombea mwili wa Balozi ikiendelea katika kanisa hilo.







 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiwaongoza Wananchi wa Zanzibar katika mazishi ya Balozi Isaac Abraham Sepetu kijiji kwa Mbuzi Unguja na kuhudhuria na Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dkt, Mohammed Gharib Bilal, Makamo wa Kwanza wa Yais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernad Membe na Viongozi wa Vyama vya Siasa na Dini Zanzibar. 
 Padri Cosmas Amani Shayo akiongoza mazishi ya Balozi Issac Abraham Sepetu katika makaburi ya Kijiji kwao Mbuzini Wilaya ya Magharibi Unguja. 
 Mwili wa Balozi Isaac Abraham Sepetu wakiwekwa katika kaburi wakati wa  maziko yake yaliofanyika katika Kijiji cha Mbuzi Unguja na kuhudhuliwa na umati wa Wananchi wa Zanzibar.
 Watoto wa marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu wakihudhuria mazishi ya Baba yao wakiwa na Mama Fatma Karume 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Balozi Sepetu baada ya mwili wa marehemu kuwekwa katika kaburi hilo wakati wa mazishi yake huko katika kijiji cha mbuzini Unguja.
Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Balozi Sepetu baada ya mwili wa marehemu kuwekwa katika kaburi hilo wakati wa mazishi yake huko katika kijiji cha mbuzini Unguja.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad,akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Balozi Sepetu baada ya mwili wa marehemu kuwekwa katika kaburi hilo wakati wa mazishi yake huko katika kijiji cha mbuzini Unguja.
 Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,akiweka mchanga katika kaburi la marehemu Balozi Sepetu baada ya mwili wa marehemu kuwekwa katika kaburi hilo wakati wa mazishi yake huko katika kijiji cha mbuzini Unguja.

 Mtoto wa Kwanza wa Balozi Sepetu Amani Isaac Abraham Sepetu, akiweka mchanga katika kaburi la baba yake baada ya kuwekwa mwili wake katika kaburi hilo wakati wa maziko yake yaliofanyika katika kijiji cha mbuzini Unguja. 
 Mtoto wa Balozi Sepetu Wema Sepetu akiwaka mchanga katika kaburi la baba yake.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatifa Bernad Membe akiweka shada la maua kumuakilishi Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya MrishoKikwete, akiwa nje ya Nchi kwa Kikazi.
 Mjane wa Balozi Sepetu Mama Amani Sepetu akiweka shada la maua katika kaburi la Balozi Sepetu wakati wa mazishi yake katika kijiji cha mbuzini Unguja.
 Mjane wa Balozi Sepetu Mama Wema Sepetu, akiweka shada la maua katika kaburi la Balozi Sepetu wakati wa mazishi yake katika kijiji cha mbuzini Unguja.
















No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.