TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Katibu Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahaman Kinana amesikitishwa na taarifa ya kifo
Cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dr Sengondo Mvungi kilichotokea Jana
katika Hospitali ya Millpark nchini Afrika ya Kusini.
Kwa niaba ya Chama Cha
Mapinduzi, Katibu Mkuu anawapa pole wanafamilia, Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Warioba na Uongozi wa Chama Cha NCCR-Mageuzi. Hakika
Taifa limepoteza Mtaalamu wa Sheria, Kiongozi Mzalendo na hodari katika kipindi ambacho mawazo yake
yanahitajika kwa kiasi kikubwa kuliendeleza Taifa hili.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali
pema peponi.
Imetolewa na:

KATIBU WA HALMASHAURI
KUU YA TAIFA
ITIKADI NA UENEZI
13/11/2013
No comments:
Post a Comment