Habari za Punde

Rais Kikwete Atia Saini Kitabu cha Maombolezi ya Dkt. Sengoro Mvungi Dar.

 Rais Jakaya Kikwete akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Dkt. Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba  akitia saini kitabu cha maombelezo ya kifo cha Mjumbe wa Tume hiyo Dkt. Sengondo Mvungi nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam.
  Rais Jakaya Kikwete (katikati) akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kushoto) nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi walipokwenda kuipa pole familia. Kulia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.


 Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Richard Lyimo akimpa pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi wakati Wajumbe wa Tume walipokwenda kumpa pole.
 Rais Jakaya Kikwete akimpa pole mke wa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, Bi. Anna Mvungi alipokwenda kumpa pole nyumbani kwake Kibamba jijini Dar es Salaam
 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba wakifurahia jambo na Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kushoto), Makamu Mwenyekiti wa Tume Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na Mjumbe wa Tume Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim (kulia) walipokutana nyumbani kwa marehemu Dkt. Sengondo Mvungi Kibamba jijini Dar es Salaam.

1 comment:

  1. Mungu ai laze mahala pema peponi, kusema kweli hilini pigo kwa wapenda mageuzi, hapa tz, tunakumbuka tangu kurudi kwa sias za mfumo wa vyama vingi dk mvungi ametoa mchango mkubwa na pengo llake hakuna ataye liziba, tunaomba vyombo vyetu vya uzinzi na usalama vihakikishe vina wapata wahalifu hawa makatili

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.