Mwakilishi wa viti maalum kupitia Watu wenye ulemavu Mhe. Zainab Abdallah Salim amewataka Wafadhili na Watu wenye uwezo kusaidia makundi maalum, ikiwemo Watu wenye ulemavu ili waweze kuepukana na hali tegemezi.
Akikabidhi Fedha taslim, Magodoro na Majiko ya Gesi kwa kikundi cha Watu wenye ulemavu Sisi tunaweza, kilichopo Muembe Makumbi kwa Hamdani amesema ameamua kuwawezesha Wanawake hao, wenye mahitaji maalum ili weze kufanya kazi zao kwa Ufanisi.
Amesema Serikali ipo Mstari wa mbele kutoa fursa sawa kwa Watu nwenye ulemavu lakini bado baadhi ya jamii hawajalipa kipao mbele suala hilo kwa Watu hao.
Aidha amesema kuna umuhimu mkubwa wa kukisaidia kikundi hicho, kutoka na kufanya kazi katika Mazingira magumu.
Kwa upande wake Mkufunzi wa Kikundi hicho bi Njuma Ali Juma amewataka Wanakikundi hao, kufanya kazi kwa bidi ili kuweza kufikia malengo walioyojipangia.
Amefahamisha kuwa, wanakusudia kuweka kituo maalum kwa wajasiriamali wanawake Wenyeulemavu lakini wakishindwa kutokana na kukosa Jengo la kwao wenyewe.
Nao wanakikundi hao, wamesema msaada huo, msaada huo umeweza kuwasaidia kwa kiasi kikubwa katika kutatua changamoto zinazowakabili na kuomba kuongezewa nguvu zaidi kwani kuna Watu wengi wenye ulemavu wanasumbuka Mitaani kutokana na kukosa kazi za kufanya.
No comments:
Post a Comment