Habari za Punde

Mabalozi Wadogo wanaowakilisha Nchi zao Wajitambulisha kwa Makamo Balozi Seif Ali Iddi.

 Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif akizungumza na Balozi Mdogo wa China hapa Zanzibar Bwana Xie Yungliang aliyefika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kujitambulisha rasmi.
  Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China Bwana Xie Yungliang akifafanua jambo kuhusu jitihada za China za kuunga mkono Zanzibar katika harakati zake za kiuchumi alipokuwa akijitambulisha kwa  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.
 Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar anayekaribia kumaliza muda wake wa utumishi Nchini Bwana Sale Suleiman Al – Harith akiipongeza SMZ na Viongozi wake kwa ushirikiano mzuri waliompa wakati wa utumishi wake hapa Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisalimiana na Balozi Mdogo wa Oman hapa Zanzibar Bwana Saleh Suleiman Al – Harith Ofisini kwake Vuga alipofika kuaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa Utumishi Nchini.(Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.