Habari za Punde

Mambo 'tiligivyogo' Skuli ya Sekondari ya Lumumba


Skuli ya Sekondari ya Lumumba, hapo zamani za kale ikijulikana kama 'Lumumba College' iko hatarini kunyofoka vipande vipande kutokana na uchimbaji mchanga uliokithiri kama unavyoonekana kwenye picha. 

Uchimbaji huu sio wa leo, yaonekana umeendelea kwa kipindi kirefu kiasi ambacho hivi sasa unahatarisha jengo zima la skuli. 

Jambo la kusikitisha inaonekana hakuna mwenye kujali. Jambo la kusikitisha yaonekana hakuna mwenye ubunifu. 

Chimba chimba mchanga nayo inaendelea, pengine hadi jengo la skuli lianguke au lianze kuota nyufa ndipo wahusika washtuke! 

Kama Lumumba ingekuwa na uongozi wenye kujali pamoja na ubunifu dawa ya uharibifu huu kwangu mimi ni ndogo tu. 

Zinunuliwe gari za mawe ambayo hayahitaji fedha za kigeni, halafu yatandikwe kwenye eneo lililochimbwa mchanga. Juu ya mawe hayo uwekwe udongo mwekundu kutoka Makunduchi au popote pale. 

Hatua ya mwisho yapandwe majani 'pemba grass'. Maji ya kila mara yamwagiwe sehemu hii na hapo tatizo limekwisha. Hili linashinda jamani?


Basi kama skuli imeshindwa kwa nini uongozi usizialike jumuiya za mazingira hapa Zanzibar na kuzipa changamoto kushughulikia eneo hili? Wakati wa kukumbatia matatizo umekwisha. 

Uongozi wa kileo unataka ushirikishaji wa jamii pale matatizo yanapotokea. Hebu tokeni humo ofisini mwende kwa wanajumuiya za mazingira na matunda yake mtayaona.

Aidha Skuli ya Lumumba mbona ina maswali mengi kuliko majibu? Mara baada ya Dkt Shein kuingia madarakani nakumbuka ilifanywa harambe kabambe yenye nia kuifanya Skuli hii kuwa 'center of excellence'. 

Nakumbuka ilikubaliwa mazingira ya Skuli yaimarishwe kwa kuzungurusha ukuta skuli yote ili kuzuia eneo na mali za skuli kuwa salama. Mapesa yaliyokusanywa yamepelekwa wapi? 

Zile juhudi za kuifanya Skuli hii kuwa 'center of excellence' zimeishia wapi? Au ndio povu la mkojo? Masikini Lumumba, kweli ndio unakufa?

4 comments:

  1. nakuunga mkono kwa hili tatizo kweli lipo kwa viongizi kutojua majukum nyinyi km walimu hamlioni hili mnangoja mtu wa nje aje kukutatulieni matatizo yenu school ilikua ni vijitega uchumi wake japo kidogo na hali ya school ilikua pia yakutizamika hivi sasa hata rangi wan asuburi wizara iwape pesa wako wapi kina maalim njeketu ,bi khadija hawa ni watu waliokua wanajua nini uingozi kweli unasikitisha hasa ukiwa umesoma hapo au unajua nini umuhimu wa elimu mwisho hii iwe kama wake up call kwa kila anae husika,

    ReplyDelete
  2. Umetaja walimu wetu waliokuwa walimu wa kweli hapo akina Nyeketu, Bi Khadija Ridhaa najua hatunae tena, Mola ampe kila lilo jema huko aliko na sijui mwalimu wangu wa Kiengereza Bi Frida yupo ama. Hii Skuli ni hazina ya Zanzibar, wanaohusika lazima waelewe majukumu yao sio ku play politic tu. Uanzishe mfuko wa kuchangia Lumumba, Lumumba School Fund. Wapo wengi waliopitia hapo ambao wangelipenda kuiona skuli hii inaendelea kung'ara.

    ReplyDelete
  3. Zanzibar imelaaniwa dhulma,choyoa,ufisadi,roho,mbaya,ushirikina,unafiki,ubinafsi,chuki na mengi tu tumekuwa kama mzuzu hatuna mbele walua nyumua u kila linalopangwa halifanikiwi kama tuloapizwa

    ReplyDelete
  4. The school I never went, Just wondering how would life turn too, had I actually attended this school..???###!!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.