Habari za Punde

Maziko ya Baba Yake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali.

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Pongwe pwani wakichukua jeneza lenye mwili wa Marehemu Baba yake Naibu Katibu Mkuuwa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,wakati wa maziko yaliyofanyika leo Kijijini hapo,Wilaya ya Kati Unguja



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Shein,akimfariji  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,baada ya kufiliwa na baba yake mzazi, na kuzikwa leo katika kijiji cha Pongwepwani Wilaya ya  Kati Unguja.

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Shein,akisalimiana na wanafamilia wa Marehemu Mzee Ali Vuai,Baba yake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,wakati wa maziko yaliyofanyika leo Kijiji cha Pongwe pawani,Wilaya ya Kati Unguja.
 Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akimfariji Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai alipofika katika kijiji cha pongwe kuhudhuria maziko hayo.  
 Katibu Mkuu wa CCM Abrahaman Kinana akiteta na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad,  wakiwa katika Kijiji cha Pongwe wakihudhuria maziko ya Baba mzazi wa  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai, yaliofanyika katika kijiji hicho na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein.
Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Silima Borafya, wakihudhuria mazishi ya baba yakeNaibu  Katibu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai yaliofanyika Kijiji kwao Pongwe.  


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Shein,(wa tatu kulia) akijumuika na Waislamu mbali mbali na Viongozi katika kulichukua jeneza la Marehemu Baba yake  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Vuai Ali Vuai,baada ya kumswalia katika Msikiti wa Ijumaa na kuzikwa Pongwepwani leo mchana

Picha na Ramadhan Othman, Ikulu

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.