Habari za Punde

Ujumbe wa Ijumaa


Mtume Muhammad Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam amesema:


 ( من ترك ثلاث جمع تهاونا طبع الله على قلبه )

Mwenye kuacha kusali Sala tatu za Ijumaa kwa mpigo kwa kutojali (na kutoona umuhimu wake) Allaah atampiga muhuri kwenye moyo wake. Muslim

Sala ya Ijumaa si jambo la khiari kwa Muislamu bali ni fardhi ya lazima     
( Fardhu ‘Ayn). 

Si sahihi kwa Muislamu kutoonesha umuhimu katika jambo Allaah Subhaanahu Wata’ala amelipa umuhimu mpaka kuamua kuupiga muhuri moyo wa mja wake abakie  miongoni mwa walio katika mghafala na kughafilika wakati kila siku tunarudi kwa Mola wetu na kumuomba ‘Ewe mwenye kubadlisha nyoyo zithibitishe nyoyo zetu katika kukutii Wewe’ Iweje nyoyo zetu zipigwe muhuri na Allaah kwa sababu ya kudharua maamrisho yake?.

Tuamke ndugu zangu katika imani na kujihimu kuitekeleza Sala ya Ijumaa kila wiki kadri ya Allaah Subhaanahu Wata’ala alivyotuwezesha kwa kutujaalia neema zake za siha, afya, uzima na uwezo wa kuitekeleza ibada hii muhimu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.