Habari za Punde

Watanzania Seattle Wamuandalia Tafrija Balozi Seif na Ujumbe wake.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitowa nasaha zake kwa Watanzania wanaoishi Seattle Washington, alipokutana nao na kuzungumzia nao wakati wa chakula cha usiku alijchoandaliwa na Jumuiya hiyo wakati wa ziara yake ya siku tano nchini humo na kufunguwa mkutano wa maonesho.
  Baadhi ya Wanajumuiya ya Watazania waishio Mjini Seattle – Washington Nchini Marekani ambao walikuwa katika tafrija ya pamoja na Ujumbe wa Kiserikali wa Zanzibar uliokuwa mjini humo kushiriki Mkutano wa 15 wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wenye asili ya Afrika wa Mji Huo ukiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi.


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania wanaoishi Seattle Nd. Yona Isimika kwenye tafrija aliyoandaliwa na Ujumbe wake Mjini Seattle.
Kati  kati yao ni Meneja Mkuu wa Benki ya Watu wa Zanzibar Limited { PBZ } Juma Amour Mohammed.

  Mtoto Hanan Masoud Kayanda wa familia za Wanajumiya ya Watanzania wanaoishi Seattle akimuuliza swali Balozi Seif kuhusu masuala ya Elimu Zanzibar ambalo lilijibiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Nd. Abdulla Mzee Abdulla aliyekuwemo pia kwenye ujumbe wa Zanzibar uliozuru Mji huo wa Kifahari.
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed hakuwa mbali katika kupiga picha ya pamoja na baadhi ya wanajumuiya ya Watanzania wanaoishi Seattle Nchini Marekani.
 Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wana kamati ya maandalizi ya Tafrika aliyoandaliwa  yeye na ujumbe wake ya Jumuiya ya Watanzania waishio Seattle.
Najisikia raha kupiga picha ya pamoja na wajukuu zangu. Alijikuta akitamka maneno hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara baada ya kuwahutubia Wanajumuiya ya Watanzania waishio Mji wa Seattle Nchini Marekani kwenye tafrija aliyoandaliwa yeye na ujumbe wake.(Picha na Hassan Issa OMPR- USA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.