Habari za Punde

Manji Achangia Mfuko wa Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya maadhimisho ya Kitaifa akipokea fedha taslim Shilingi Milioni 15,000,000/- kutoka kwa  Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group Bwana Yussuf Manji kuchangia sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group ambae pia ni Mwenyekiti wa Kalabu ya Soka ya Yanga ya Dar es salaam Bwana Yussuf Manji mara baada ya kupokea mchango wa mfanyabiasra huyo nyumbani kwake Mazizini Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.(Picha na Hassan Issa  OMPR) 

3 comments:

  1. nakusikitia nd manji kwa kupoteza fedha hizo kwa mambo ya sherehe, laiti ungewadhamini wanafunzi wakimaskini ambao hawawezi kujilipita karo za vyuo ungekuwa umefanya la maana , au ungepeleka kwenye hospitali yoyote ya walalahoi ungekuwa umejiwekea bima ya uhakika kwa Mtukufu Mungu kwa kuwasaidia wagonjwa , tumeweka mbele kujipendekeza kwa watawala na wanasiasa ambao wenyewe wamejaa dhuluma tupu, tunawacha kujipendekeza kwa muumba mwenye uwezo usio mpaka , lakini wapii aliyepotea huwezi kumwongoza

    ReplyDelete
  2. Kama hujui huyu ndie aliepewa tenda ya kuendeleza lile eneo la bwawani linalowekwa makontena kwa kulijenga maduka.

    Inaskitisha kusikia kua Bakhressa alinyimwa eneo lile eti kwa kua msimamo wake wa kisiasa sio mzuri a.k.a 'sio mwenzetu' lakini tunasahau kua anaongoza kwa kuchangia maendeleo!

    Ndugu yangu hakuna Muhindi aliye tayari kupoteza fedha zake bure hasa ukizingatia hasira walizo nazo baada ya mali zao nyingi kutaifishwa baada ya mapinduzi na azimio la Arusha kwa kule Bara

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.