BAADHI ya Bidhaa za Mafuta ya Memei zilizotengenezwa katika kiwanda cha Makonyo Wawi kupitia Wataalam wa Kampuni ya Land Co.ya Japani.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe. Nassor Ahmeid Mazrui,akiangali moja ya Bidhaa ya Mafuta ya Mimea iliotengenezwa na Kampuni ya Land Co. ya Chumvi maalum ya kuogea
MAOFISA wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar wakishuhudia utilianaji wa saini hiyo ya makubaliano ya mradi wa kuzalisha bidhaa za Mafuta ya Mimea kati ya ZSTC na Land Co ya Japan.
RAIS wa Kampuni ya Land Co.ya Japan Bwa. Akira Abe, akitowa maelezo ya mradi huo wa utengenezaji wa Mafuta ya Mimea wakati wa utilianajin wa saini ya mradi huo uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya ZSSF Tibirinzi Chakechake Pemba.
WAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko Mhe.Nassor Ahmeid Mazrui, akizungumza katika hafla hiyo ya utilianaji saini ya mradi wa Utengenezaji wa Mafuta ya Mimea, hafla hiyo imefanyika ukumbi wa Hoteli ya ZSSF
BALOZI wa Japan Nchini Tanzania Bwa. Mafaki Okada, akizungumza katika hafla hiyo ya utilianaji wa saini kwa pande mbili za ZSTC na Land Co ya Japan.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Biashara la ZSTC Zanzibar Bi Mwanahija Almas Ali akitowa maelezo ya makubaliano ya mradi huona Land Co ya Japan na Shirika la la SZTC, wakati wa utilianaji wa saini ya makubaliano ya mradi huo wa kuzalisha Mafuta ktumia mimea .
MKURUGENZI Muendeshaji wa Shirika la Biashara Zanzibar ZSTC Bi Mwanahija Almas , akitiliana saini na Rais wa Land Co, ya Japan Bwa. Akira Abe, makubaliano ya pande hizo mbili katika mradi wa pamoja utengenezaji wa Mafuta ya Mimea kutoka Zanzibar, makubaliano hayo yamefanyika katika ukumbi wa ZSSF Kibirizi Pemba, wakishuhudia Balozi wa Japani Nchini Tanzania Mafaki Okada na Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Nassor Ahmeid Mazrui.
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Nassor Mazrui na Balozi wa Japan Nchini Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SZTC na wa Ubalozi wa Japan na Kampuni ya Land Co.
No comments:
Post a Comment