Habari za Punde

Uzinduzi wa KituoKipya cha Ununuzi wa Karafuu Chambani ikiwa ni Sherehe za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar

 Jengo jipya la Kituo cha Kununulia Karafuu katika Kijiji cha Chombani Wilaya ya Mkoani Pemba kilichofunguliwa na Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Mhe. Nassor Ahmeid Mazrui. 
 Mhe Nassor Mazrui akiondosha kitambaa kuashiria kukifungua Rasmin Kituo Kipya cha Ununuzi wa Karafuu cha Shirika la Biashara la Taifa ZSTC,katika kijiji cha Chambani Wilaya ya Mkoani Pemba.
 Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmeid Mazrui, akikata utepe kuashiria kukizindua Kituo kipya cha Ununuzi wa Karafuu katika Kijiji cha Chambani Wilaya Mkoani Pemba, anayeshuhudia Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC, Bi. Mwanahija Almas.uzinduzi huo ni moja ya sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kutimia miaka 50ya Mapinduzi.. 
 Waziri wa Biashara Mhe. Nassor Mazrui, akiangalia karafuu zilizoletwa na Mkulia katika kituo hicho kwa ajili ya kuziuza akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Muendeshaji wa ZSTC Mwanahija Almasi

Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Zanzibar Nassor Mazrui, akitembelea kituo hicho baada ya kukifungua rasmin kwa ajili yaWakulima wa Zao hilo la Taifa kutumia kituo hicho kilichoko karibi na Makazi yao Chamani Wilaya ya Mkoani Pemba. 
Waziri Mhe.Mazrui akiangalia karafuu zilizouzwa kwa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSTC Mwanahija Almas, baada ya muda mfupi kukifungua rasmin ikiwa n shamrashara za Mapinduzi kutimia miaka 50.. 
 asoma utenzi wakisoma utenzi wa uzinduzi wa Kituo cha ununuzi wa Karafuu Chamani Pemba.
Mambo ya Chamani hayo wakati wauzinduzin wa kituo hicho cha ununuzi wa karafuu, Waziri akipata sadaka ya Haluwa katika tafrija hiyo, ukifika Pemba upate radha ya haluwa ya Pemba uone utamu wake Mdau   
Wadau wa Karafuu kongeni mioyo kwa haluwa ndivyo inavyoonekana akisema mdau huyu wa ZSTC alipokuwa akigawa haluwa hiyo kazi kwako. Mkulima wa Karafuu wakati ni Huu peleka karafuu zako ZSTC, Bei yake iko Juu wachana na Walaguzi wa Zao hilo kwa kununu kwa Pishi ya bint Hole.Mnunuzi ni mmoja tu ni ZSTC PEYEE .  
Waziri wa Biashara Viwanda na Masoko Nassor Ahmeid Mazrui, akizungumza na Wananchi wa Chambani wakati wa Sherehe za Ufunguzi wa Kituo kipya cha Ununuzi wa Karafuu Chambani Wilaya ya Mkoani Pemba na kuwataka karafuu zao kuziuza kwa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ZSTC, Kituo hicho tangu kuaza kutowa huduma ya Ununuzi wa Karafuu tayari kimeshanunua Tani 42 za Karafuu kavu.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar Mwanahija Almas Ali, akitowa maelezo ya Ujenzi wa Kituo hicho cha Ununuzi wa Karafuu kwa Wananchi wa Wilaya ya Mkoani Kijiji cha Chambani, ili kupunguza masafa ya kufata vituo vilioko mbali na makazi yao.   
 Mwananchi wa Kijiji cha Chambani akisoma risala ya Wakulima wa karafuu katika kijiji hicho wakati wa hafla ya uzinduzi wa kituo chao cha ununuzi wa karafuu, na kufarijika na ujenzi wa kituo hicho kimewapunguzia masafa ya kufuata vituo viliko mbali na makazi yao na kupata ufumbuzi wa tatizo hilo kwa kujegewa sehemu muafaka kwao.

Viongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar wakifuatlia sherehe za Uzinduzi wa Kituo cha Ununuzi wa Karafuu Chambani wakati wa ufunguzi wake Kijiji hapo.
Karani wa kituo Kipya cha ununuzi wa karafuu Chambani wakimuandikia risiti mkulima aliyeuza karafuu zake katika kituo hicho baada ya uzinduzi wake uliofanywa na Waziri wa Biashara Mhe. Nassor Mazrui. 
Wakulima wa zao la karafuu wakiwa katika kituo cha ununuzi wa karafuu wakisafisha karafuu zao wakisubiri kupimiwa na kupewa gred wakiwa katika kituo cha chambani  

Wafanyakazi wa Shirika la Biashara la Taifa ZSTC wakipima karafuu ambazo zimenunuliwa na ZSTC kwa wakulima wa Kijiji cha Chambani.
Vijana wa Kijiji cha Chambani wakicheza ngoma ya Kibati katika sherehe za Uzinduzi wa Kituo Kipya cha Ununuzi wa Karafuu Chamani Wilaya ya Mkoani Pemba.
Watoto Abdalla Mohammed na Suleiman Mohammed ambo wete ni ndugu wakionesha umahiri wao wa kucheza ngoma ya kibati kwa wananchi wa chambani wakati wa uzinduzi wa kituo kpya cha ununuzi wa karafuu chamani wilaya ya mkoani Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.