HOTUBA
YA UFUNGUZI WA MRADI WA MAFUTA YA MIMEA KATIKA UKUMBI WA ZSSF, TIBIRINZI,
CHAKE
CHAKE, PEMBA
SIKU
YA JUMAANE, DISEMBA 17, 2013.
MRADI
ZSTC
- ZANZIBAR & LAND CO. LTD.,- JAPAN
Mkurugenzi Muendeshaji wa SZTC Bi Mwanahija Almas Ali
NDUGU
MGENI RASMI, BALOZI WA JAPAN ,
NCHINI TANZANIA MHESHIMIWA MAFAKI OKADA,
MHE. WAZIRI WA BIASHARA,
VIWANDA NA MASOKO WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR , MHE AHMED NASSOR MAZRUI.
MHE. NAIBU WAZIRI WA BIASHARA,
VIWANDA NA MASOKO WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR , MHE. THUWAYBA KISASI.
MHESHIMIWA KAIMU MKUU WA MKOA
KUSINI, PEMBA MHE DADI FAKI DADI,
NAIBU KATIBU MKUU WIZARA
YA BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO, BW RASHID SALIM.
MWAKILISHI WA JETRO KUTOKA
NAIROBI BW.
HIROSHI KOMATSUZAKI.
MWENYEKITI WA BODI YA ZSTC,
BW KASSIM SULEIMAN PAMOJA NA WAKURUGENZI
WENZAKE.
RAIS WA LAND CO. YA JAPAN,
BW. AKIRA ABE
MAAFISA KUTOKA UBALOZI WA
JAPAN NA LAND CO.
MAAFISA WADHAMINI WA
WIZARA MBALI MBALI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR .
WAKURUGENZI WA IDARA NA
TAASISI MBALI MBALI ZA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR .
WAKUU WA IDARA MBALI MBALI NA WAFANYAKAZI WA Z.S.T.C.
WANAHABARI WA VYOMBO VYOTE
VYA SERIKALI NA BINAFSI.
WAPENZI
WAGENI WAALIKWA MABIBI NA MABWANA.
ASSALAAM ALAYKUM.
MHESHIMIWA
MGENI RASMI NA WAHESHIMIWA WAGENI WAALIKWA.
AWALI YA YOTE HATUNA BUDI KUMSHUKURU ALLAH ALIYETUJAALIA
SIKU YA LEO HII KUFIKA HAPA SALAMA TUKIWA WAZIMA NA WENYE AFYA NJEMA.
NAPENDA KUCHUKUA NAFASI
HII KUMSHUKURU MHE. BALOZI MAFAKI OKADA NA UJUMBE WAKE KWA KUKUBALI KUWA
NASI SIKU YA LEO KATIKA HAFLA YETU HII MUHIMU IKIWA NI SEHEMU YA UTEKELEZAJI WA
MAGEUZI YANAYOENDELEA KUTEKELEZWA NA SHIRIKA. NA VILE VILE IKIWA NI SEHEMU YA
SHAMRA SHAMRA ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MAPINDUZI, ZANZIBAR .
HALKADHALIKA NAMSHUKURU WAZIRI
WETU MHE. AHMED NASSOR MAZRUI AMBAE ANA MAJUKUMU MENGI YA KIKAZI, KWA KUYAACHA
NA KUJA KUUNGANA NASI.
PIA SHUKRANI ZIMWENDEE
NAIBU WAKE MHE. MAMA THUWAIBA KISASI KWA AMBAE PAMOJA NA KUKABILIWA NA MAJUKUMU
MBALI MBALI IKIWAMO KIKAO CHA B. L. W KINACHOENDELEA HIVI SASA NAE KWA KUPATA
NAFASI YA KUJUMUIKA NASI.
AIDHA, NAMSHUKURU KAIMU MKUU
WA MKOA KUSINI VILE VILE KWA KUJUMUIKA NASI KATIKA HAFLA HII.
PIA NATOA SHUKRANI ZA
DHATI KWA MWAKILISHI WA JETRO KANDA YA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA NAIROBI BW
HIROSHI KOMATSUZAKI, NA RAIS WA LAND CO. BW. AKIRA ABE.
VILE VILE SHUKRANI
ZIWAENDEE WAKURUGENZI WA BODI YA SHIERIKA, MAAFISA WADHAMINI WA WIZARA MBALI
MBALI, WAKURUGENZI WA TAASISI NA IDARA MBALI MBALI, WAKUU WA IDARA NA
WAFANYAKAZI WA SHIRIKA, KAMATI YA MAANDALIZI, WANAHABARI WOTE NA WAGENI WOTE
WAALIKWA.
MHESHIMIWA
MGENI RASMI NA WAHESHIMIWA WAGENI WAALIKWA
SHIRIKA LA BIASHARA LA
TAIFA NI SHIRIKA LENYE HISTORIA NDEFU KATIKA USIMAMIZI WA UZALISHAJI, UNUNUZI
NA UUZAJI WA KARAFUU NA MAFUTA YA MIMEA.
NI SHIRIKA PEKEE LILILOPEWA MAMLAKA NA SERIKALI KUFANYA HIVYO. NA NI WAMILIKI
WA KIWANDA PEKEE KINACHOZALISHA MAFUTA YA MIMEA HAPA ZANZIBAR ,
KIWANDA HICHO KIPO PEMBA NA KIMEANZISHWA MIAKA
30 ILIYOPITA.
KWA SASA SHIRIKA LIKO
KATIKA MCHAKATO WA MAGEUZI, AMBAYO YATACHUKUA MIAKA KUMI KUANZIA 2011 HADI 2021.
MAGEUZI HAYA YAMETOKANA NA
TAFITI MBALI MBALI ZILIZOFANYWA NA SERIKALI ILI
KUTATUA MATATIZO YA SEKTA YA KARAFUU NA KUZIKABILI CHANGAMOTO ZAKE.
VILE VILE MAGEUZI HAYO
YATAGUSA KUREKEBISHA MFUMO WA UENDESHAJI SHIRIKA. MAENEO MENGINE YATAKAYOGUSWA
NA MAGEUZI HAYO NI UZINDUZI WA MRADI HUU
WA LEO.
MHESHIMIWA
MGENI RASMI NA WAHESHIMIWA WAGENI WAALIKWA
MOJA YA FAIDA ZA MRADI HUU
WA LEO ITAKUWA NI KUKIDHI MAHITAJI YA SOKO AMBAYO HUBADILIKA KUENDANA NA WAKATI
HUSIKA.
MHESHIMIWAM
MGENI RASMI NA WAHESHIMIWA WAGENI WAALIKWA
MHESHIMIWA
MGENI RASMI NA WAHESHIMIWA WAGENI WAALIKWA
NAOMBA NITOE MAELEZO
KUHUSIANA NA HAFLA HII YA LEO, HUU NI MRADI WA MASHIRIKIANO YA KIBIASHARA KATI
YA Z.S.T.C. NA LAND CO., YA JAPAN KATIKA KUIMARISHA NA KUENDELEZA BIDHAA ZA
MAFUTA YA MIMEA YANAYOZALISHWA NA SHIRIKA.
CHIMBUKO LA MRADI HUU
LIMETOKANA NA MAONYESHO YA “COSME TOKYO ”
YANAYOFANYIKA JAPAN
KILA MWAKA. SHIRIKA LILIHUDHURIA MAONYESHO YA JUNI, 2012 NA JUNI, 2013. KATIKA
MAONYESHO HAYO, MAAFISA WA SHIRIKA WALIKUTANA
NA RAIS WA LAND CO., NA KUFANYA MAZUNGUMZO YA KINA KUHUSIANA NA MASHIRIKIANO NA
MRADI HUU.
MAZUNGUMZO HAYO, YAMEZAA
MATUNDA YANAYOASHIRIA MRADI KUWA NA MANUFAA KWA PANDE ZOTE MBILI.
MRADI HUU UNAOZINDULIWA
LEO UTAKUWA NI WA MUDA WA MIAKA 3 NA UNADHAMINIWA
NA ZSTC, LAND CO. NA KUSAIDIWA NA SHIRIKA LA BIASHARA ZA NJE LA JAPAN (JETRO) NA
UTAKUWA NA MADHUMUNI MAKUBWA YAFUATAYO:
1.
KUIMARISHA KWA KUZIONGEZA THAMANI BIDHAA ZA
SHIRIKA.
2.
KUTOA AJIRA KUTOKANA NA UANZISHWAJI WA
VIWANDA VIDOGO VIDOGO KWA LENGO LA KUPUNGUZA UMASIKINI
3.
KUZIWEZESHA BIDHAA ZA SHIRIKA KUUZWA KATIKA
SOKO LA JAPAN
NA MASOKO MENGINE YA NJE.
4.
KUWEZESHA SHIRIKA KUTANUA SOKO LA NDANI KWA
BIDHAA HIZO.
5.
KUTOA ELIMU ELEKEZI, UJUZI WA KITAALAMU NA
MAFUNZO STADI KATIKA UANZISHWAJI WA
VIWANDA VIDOGO VIDOGO, ZANZIBAR .
6.
KUZALISHA BIDHAA ZENYE VIWANGO
VINAVYOKUBALIKA KIMATAIFA.
MHESHIMIWA
MGENI RASMI NA WAPENZI WAALIKWA,
NAOMBA NISEME KWAMBA, NI
IMANI YETU MRADI HUU UTAKUWA NA TIJA NA UTATOA MWANGA MBELE TUENDAKO KUTOKANA
NA JITIHADA KUBWA ZITAKAZOFANYWA KWA MASHIRIKIANO YETU ZSTC NA LAND CO. YA
JAPAN.
TUNAAHIDI KUFANYAKAZI KWA
PAMOJA NA LAND CO. KWA UWAZI
(TRANSPARENCY), MFUMO BORA WA UENDESHAJI (SOUND MANAGEMENT) NA UWAJIBIKAJI
(ACCOUNTABILITY).
WAHESHIMIWA MLIOHUDHURIA
HAPA LEO MTASHUHUDIA UWEKAJI SAINI WA MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO YA KIBIASHARA
BAINA YA Z.S.T.C. NA LAND CO., YA JAPAN .
NAISHUKURU WIZARA YA
BIASHARA, VIWANDA NA MASOKO PAMOJA NA AFISA MDHAMINI WAKE KWA KUWA KARIBU NASI
KATIKA KUTEKELEZA MRADI HUU.
MHESHIMIWA
MGENI RASMI NA WAHESHIMIWA WAGENI WAALIKWA,
NAWASHUKURU NYOTE KWA MARA
NYENGINE TENA KWA MAHUDHURIO YENU, ENDAPO KUNA KASORO YO YOTE ILIYOJITOKEZA
NAPENDA KUOMBA RADHI KWA HALI HIYO NAOMBA ICHUKULIWE KUWA NI KASORO ZA KIBINADAMU
NA SIO MAKUSUDIO YETU.
AHSANTENI
KWA KUNISIKILIZA.
No comments:
Post a Comment