JUKAMKUM/BR/1/VOL.1/62 Date: 18/12/2013
RISALA FUPI KWA MGENI RASMI
MAKARIBISHO
MH: MGENI RASMI
Kwa
niaba ya wanachama, Viongozi na Vijana kwa pamoja tunatoa shukrani zetu za
dhati kwako, kwa kuamua kuja kuitembelea Jumuiya inayotoa Elimu kwa jamii
kuhusu Athari za Madawa ya Kulevya, Ukimwi, Mimba katika umri mdogo (JUKAMKUM).
Tunaamini
kuwa unazo shughuli nyingi za Kitaifa ambazo zina umuhimu mkubwa, lakini
umeamua kuzibakisha hadi baadaye, tunasema ahsante sana na karibu JUKAMKUM.
MH: MGENI RASMI,
Fursa
hii tulikuwa tunaisubiri kwa hamu kubwa na leo tumeipata, tunaamini ndani ya
nyoyo zetu kuwa Jumuiya hii inatambulika na itaendelea kutambulika ndani ya
nchi na nje ya nchi, pia itapata baraka zenye kheri, tunakuombea dua kwa
Mwenyezi Mungu akupe kila la kheri, akuepushe na matatizo yote ya dunia wewe
pamoja na familia yako yote Ameeen.
MH: MGENI RASMI,
Jumuiya
hii imeanzishwa 08/06/2002 na kupata
usajili 20/08/2008 kwa hati ya usajili namba 579, afisi ya Jumuiya ipo hapa Pemba katika Wilaya ya Chake Chake.
MH: MGENI RASMI:
Kila jambo linakuwa na sababu
ya kuwepo kwake, hivyo lengo la jumuiya hii ni kama
ifuatavyo:
1.
Kupunguza
utumiaji na athari za dawa za kulevya.
2.
Kupunguza kasi ya
maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi na ukimwi wenyewe
3.
Kupunguza tatizo
la watoto wa kike kupata mimba katika umri mdogo au zisizo tarajiwa.
4.
Kupambana na
maradhi nyemelezi ikiwemo TB.
MWELEKEO WA JUMUIYA:
ND. MGENI RASMI.
Jumuiya
inashirikiana na itashirikiana na taasisi husika za Serikali na zisizo za
kiserikali katika kupunguza ongezeko la utumiaji wa dawa za kulevya, maambukizi
mapya ya virusi vya ukimwi na ukimwi, pamoja na watoto wa kike waepuke kupata
mimba katika umri mdogo.
MAFANIKIO:
Tulipata
ruzuku ndogo kutoka The Foundation for
Civil Society Tanzania Bara, ambapo ruzuku hii ilitumika kwa kuwapa elimu Vijana 80 wanaotumia dawa ili kujitambua.
Baada
ya mafunzo hayo, vijana 15 waliamua
kuacha kutumia dawa na sasa wanaelimisha wenzao waache kutumia dawa hizo.
Jumuiya
ilianzisha Dropping Center kwa ajili ya kuwaelimisha vijana namna ya kujielewa
na kujua wako wapi na wanahitaji kufika wapi na baada ya kuelewa dhana nzima ya
kuwepo kwao duniani na kuwa wako ambao wanawategemea, tumeweza kuanzisha (Soba
house) sehemu ambayo vijana hubakia humo kwa muda wa miezi mitatu mpaka mine ili
kuweza kupata mafunzo ya jinsi ya kubadilisha tabia, kukabiliana na changamoto
za hamu ya dawa ili kuweza kurejea kama
mwanzo. Kwa sasa JUKAMKUM ina soba house tatu mbili zikiwa Wilaya ya Chake
chake na moja Wilaya ya Mkoani.
Jumuiya imepata tunzo ya kuwa
asasi bora kupitia The foundation for Civil society kwa mwaka 2012/2013.
Jumuiya inapata mashirikiano
ya karibu sana
na Viongozi wa Wilaya, Jamii husika na maafisa Wadhamini wa Wizara mbalimbali.
CHANGAMOTO ZA JUMUIYA:
1. Jumuiya imekabiliwa na tatizo la nyenzo zikiwemo fedha
ambapo vijana waliopo wanahitaji kupata huduma za lazima kama ,
kula, kulala na matibabu ambapo baadhi ya wazee wanaweza kusaidia gharama
lakini wengine hawamudu.
2.
Majengo
ambayo tunatumia kama soba house ni majengo ya
kukodi, muda wa kodi umekaribia kumaliza na Jumuiya haina uwezo wa kumudu kwani
gharama zake ni kubwa. Kwa hili tunaomba kwako kama
Mzee utuangalie kwani jengo hili ambalo leo tupo hapa kodi yake inamalizika
mwezi huu wa Disemba na mpaka sasa hatuna chanzo cha kuweza kupata gharama za
kulipia kodi ya mwaka unaofuata.
3. Pamoja na kuwasaidia vijana katika kukabiliana na
tatizo la utumiaji wa dawa za kulevya JUKAMKUM mpaka sasa haina mradi wa
kuwaendeleza vijana wakaweza kuwa na angalau chanzo kidogo cha mapato.
JUKAMKUM
inapenda kuchukua fursa hii kuomba kupatiwa nyenzo kwa ajili ya uanzishaji wa mradi wa ufugaji wa kuku na mbuzi kwa vijana walio
katika vituo vyetu ambao kwa kiasi fulani mapato yake yanaweza kutumika
kusaidia huduma za soba na kuwawezesha vijana kupata uzoefu wa ufugaji ambao
wanaweza kuutumia katika jamii watakapotoka katika vituo hivi.
ND.
MGENI RASMI:
Kwa
kumalizia tunatoa tena shukurani zetu kwako na kwa wale wote ambao mmefika hapa
kututembelea. Mwenyezi Mungu awajaalie
afya njema na pia awarudishe salama nyumbani na katika ziara zenu nyengine ili
kuendeleza mbele Taifa letu kwa ujumla.
Ahsanteni sana .
No comments:
Post a Comment