Na Fatuma Kitima, DSM
TAKWIMU zinaonesha kumekuwa na ongezeko la matukio 264 ya ajali za
barabarani kwa mwaka jana ambapo ni sawa na asilimia 1.1, ikilinganishwa na mwaka 2012
ambapo matukio yalikuwa 23,578.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, alitaja maeneo
aliyoongoza kwa ajali ni
Kinondoni,Ilala, Temeke Kilimanjaro na Pwani.
Alisema ajali zilizosababisha vifo kwa mwaka 2013 ni 3,427 sawa na
ongezeko la asilimia 3.0 ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo kulikuwa na
vifo 3,328.
Alisema kuwa ajali zilizosababisha majeruhi kwa kipindi hicho ni 11,307 sawa na ongezeko la asilimia 2.6
ikilinganishwa na mwaka 2012 ambapo kulikuwa na majeruhi 11,021.
Alianisha kuwa kumekuwa na
ongezeko la vifo 33 sawa na asilimia 0.8 kwa mwaka jana ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2012 ambapo
kulikuwa na vifo 3,969, hata hivyo kumekuwa na ongezeko la majeruhi 578 kwa
mwaka 2013 sawa na asilimia 2.9 tofauti na mwaka 2012 ambapo kulikuwa na
majeruhi 20, 111.
Alisema kuna baadhi ya mikoa ambayo imepunguza idadi ya ajali
ikiwa ni Arusha, Mwanza,Mbeya na
Morogoro.
Alibanisha kati ya makundi
hayo, ajali za pikipiki zimeongoza kwa
ajali nyingi ambapo takwimu zinaonesha idadi ya ajali kwa mwaka 2013 ni 6,831 sawa na asilimia 18.5
tofauti na mwaka 2012 ambapo kulikuwa na ajali 5,763.
Alisema idadi ya ongezeko la vifo vilivyotokana na pikipiki kwa mwaka
2013 ni 168 sawa na asilimia 18.1 ambapo mwaka 2012 kulikuwa na vifo 930, hata
hivyo kwa mwaka 2013 kumekuwa na ongezeko la
majeruhi 1,046 sawa na asilimia 19 ambapo mwaka 2012 kulikuwa na
majeruhi 5,532.
Kutokana na ongezeko hilo polisi imepanga mikakati mbalimbali ya
kupunguza ajali za barabarani kwa mwaka 2014 ambazo ni ushirikishwaji kwa jamii
na elimu kwa umma ambapo watapanua wigo wa utoaji elimu kwa umma ikiwa ni
pamoja na kuboresha mipango katika vipindi vya redio na televisheni.
Aidha alisema kutakuwa na uthibiti wa makosa ikiwa ni pamoja na kuongeza
ukamataji wa madereva wasiopenda kutii sheria bila shuruti, matumizi ya liseni
mpya kudhibiti mienendo ya madereva na kuongeza matumizi ya teknolojia na
mawasiliano.
No comments:
Post a Comment