Kauthar Abdalla na
Salum Simba, MUM
WAZIRI wa Katiba na
Sheria, Mhe. Aboubakary Khamis Bakary, amesema kumekuwa na migogoro mingi
misikitini inayosababishwa na michango inayoingia kutoka vyanzo mbali mbali,
ikiwemo vitega uchumi.
Aidha alisema
migogoro mengine inasababisha na tofauti za kifikra, elimu na mitazamo.
Akiwasilsha ripoti
ya utekelezaji wa maagizo ya kamati ya Katiba, Sheria na Utawala ya Baraza la
Wawakilishi ya mwaka 2012/2013, Waziri huyo alisema, hata hivyo wamechukua juhudi kuonana na
viongozi wa misikiti kwa kushirikiana na taasisi ya World Islamic Call Society
kutoka Libya.
Kuhusu uajiri
katika ofisi ya Msajili wa Hakimiliki, alisema wizara imeajiri watendaji watatu
na tayari wameshaanza kazi katika mwaka wa fedha 2013/2014.
Aidha alisema
wizara bado inaendelea na juhudi za kupata hakimiliki za jengo la taasisi hiyo
kisiwani Pemba kwa sababu haipo na hata baada ya kufuatilia wizara
inayoshughulika na ujenzi imekosekana.
Akiwasilisha ripoti
ya Kamati hiyo, Mwenyekiti wake,
Mhe.Ussi Jecha Simai, alisema kamati imepata taarifa za kusikitisha kuhusu wizi
wa nyaraka muhimu uliotokea katia idara ya nyaraka.
Alisema wizi huo
umekuja kutokana na kutokuwepo kamera za usalama (CCTV) ambayo licha ya
kupigiwa kelele muda mrefu wizara
imeshindwa kuweka kamera hizo hadi wizi huo ulipotokea.
Akigusia Tume ya
Kurekebisha Sheria, Mwenyekiti huyo aliitaka serikali kutilia mkazo suala la
upatikanajai wa jengo la ofisi pamoja, ufinyu wa bajeti na kuongeza maslahi ya
watumishi wa tume hii kwa sababu wanafanya kazi ngumu.
Kwa upande wa ofisi
ya Mkurugenzi wa Mashtaka, alisema watumishi wanne wameshakimbia ambao
wamehamia taasisi nyengine kufuata maslahi bora.
Aidha aliishauri
serikali kuyafanyia ukarabati majengo ya Idara ya mahakama ambayo yanaonekana
kuchakaa na kujipanga kujenga mengine mapya.
Kamati hiyo
ilisikitishwa na vitendo vya baadhi ya majaji kupuuza taratibu zilizopo kwenye
sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai, ambapo baadhi yao ni wale
waliolalamikiwa na Jumuiya ya Wanasheria Zanzibar (ZLS) baada ya kuteuliwa na
Rais mwaka 2010.
Alisema hoja kuwa
ni uwezo wao mdogo na wengineuadilifu wao katika kuendesha mashauri mbali mbali
ni wa mashaka.
Alisema yapo
mashauri mengi katika mahakama za watoto ambayo yalipelekwa muda mrefu bila
kusikilizwa na mengine kufutwa kutokana na wazee kuchoka kusubiri.
« Lipo shauri
limefutwa kwa sababu mtoto aliyefanyiwa udhalilishaji ameshafikia umri ambao ni
zaidi ya umri aliokuwa nao wakati akifanyiwa udhalilishaji na mzee wake kuamua
kutoendelea na kesi hiyo, » alisema.
Alisema pia yapo
makosa ya ubakaji na udhalilishaji kijinsia yaliyopewa hukumu ambazo zipo
kinyume na sheria, ikiwemo mshitakiwa kulipishwa faini ya shilingi 400,000
ambapo muathirika alipewa shilingi 100,000.
Wakichangia, wajumbe
wa baraza la Wawakilishi wameiomba serikali kuweka mahakama maalum za
kusikiliza kesi zinazohusiana na migogoro ya wawekezaji ili kutoa uhuru zaidi
wa kuendesha kesi hizo.
Aidha walisema
idara ya mahakama inategemewa zaidi kutoa haki hivyo mahakimu na majaji watoe
hukumu kwa mujibu wa sheria.
Mwakilishi wa
Kitope, Mhe. Makame Mshimba Mbarouk, alisema kumekuwa na malalamiko mengi
kwamba mahakama hazitekelezi majukumu yake ipasavyo hali inayosababisha kuongezeka migogoro.
No comments:
Post a Comment