Habari za Punde

Mdau wa ZanziNews na ushauri wake


Asalaam Alaykum kaka Othman!

Ni matarajio yangu kuwa umzima na waendelea kulisukuma gurudumu  la utoaji habari kama kawaida kupitia katika nyanja zako kiilivyo na bado hujawa "mzigo kwa taifa".

Wajuwa kaka Othman,mimi hujisikia raha sana ninapoingia katika blog yako na kuanza kusoma habari za huko nyumbani.Hujihisi nipo poa kabisaaa lakini yajitokeza siku hizi kuwa blog yako yanivunja moyo na baadhi ya nyakati hujenga mawazo ya kuwa hamna mpya hasa. Maana ninapofungua hukuta habari "uporo" ambapo nyengine hubakia kama kwa siku 3-4. Waswahili wansema kipya kinyemi lakini kikuukuu kama ni kilaji huwa uporo na kama ni nguo huwa mtumba. Kiujumla kwa yote mawili hadhi na haiba hupungua kwa mtumiaji.

Ninachokushauri kama hamna (yaani wewe na crews) wako lakutuwekea jipya basi mie naona bora mbadilishe jina la blog yenu na kuiita zanzibar weekly news. Tutajuwa wasomaji kuwa twasoma habari za juma zima lililopita au tulilonalo. 

Wajuwa masikio na macho yetu hujawa na mshawasha zaidi kusoma au kuona habari moto mto (mpya) yaani breaking news na ndipo kunakofanya kila wakati kutembelea blog lako lakini vyenginevyo ham na utwashi wa kutembelea huondoka. Jee itakuwa ni fahari kwako lipi kati ya mawili hayo kwa mtembeleaji wako blog hii awenalo.

Mimi siamini kuwa zanzibar (Unguja na Pembae) kuwa kuna uhaba wa habari moto moto mbona "mawio" wao hawazikosi,jee wao wanzitoa wapi,kulikoni !. Jaribuni ku up-date mara kwa mara kama wafanyavyo wakina Issa Michuzi ambapo ukikawia tu mada yayoyoma huikuti na kitu kipya chawekwa.

Nadhani kwa hayo ingawa ni mengi na nadhani hayakukuchosha kuyasoma namalizia kwa kusema kuwa kaza kamba ili haiba ipatikane katika blog yako.

 Shukran na Wasalaam.

3 comments:

 1. kadha buti kaka zanzinews ,usipotezee muelekee ,huyo mdau anakupenda

  ReplyDelete
 2. aliyokueleza huyu mdau ni ya kweli kabisa; na nataka nikwambie jambo kuhusu hiki kinachoitwa habari; hasa hasa kwa sisi tulioko ughaibuni ile kutuwekea tu picha kwa mfano wa maeneo mbali mbali ya huko Zanzibar basi ni habari tosha; na amini usiamini hutumia muda mwingi kuziangalia picha hizo na kutukumbusha maeneo hayo ambayo aghalabu huwa tunayajua vizuri; hapo ni picha tu bila hata habari yoyote maalum; kuonesha tu yale maeneo ya vitongoji na mitaa ya Zanzibar; lakini pia unaweza Kaka othman pale ambapo kuna upungufu wa news moto moto ya kutundika kwenye blog yako, unaweza kutuwekea twasira zinazoonesha matukio ya sasa hivi hapo mjini zanzibar; unaweza kwamfano ukaweka taswira mwanana ukaandika hivi ni kama tulivyoidaka mida hii ya mchana kwenye soko la mboga mboga la kiembesamaki; au hii taswira tumeinasa muda mdogo uliopita kwenye kutuo kipya cha dala dala cha kiswandui; au taswira mwanana inaonesha mandhari ya forodhani leo jioni nk nk nk kwa namna hii unajikuta kila wakati una cha kutundika si lazima ziwe habari moto moto; niamini ukifanya haya na mengine blog yako itaongezeka wasomaji na wapenzi mpaka useme basi! huo ni ushauri wa bure kaka - kazi kwako!

  ReplyDelete
 3. Na mimi wacha nichangie kwa ajili ya kumpa tough mwenzetu na aboreshe kazi yake na kwa upande mwengine na sisi tuendelee kupata habari, kuburudika na pia kuelimika. Mzee Mapara amekuwa ni kiungo kikubwa kwetu katika kuyafikia hayo niliyoyasema hapo, mimi mwenyewe nimekuwa namtumia habari na issues za kupost na hana noma anapost tu, nikiwa hapa Zanzibar na nikiwa nje ya nchi ndio kabisa nabrowse almot all the time on his blog. Habari zake kweli huwa zina mgando na zinachelewa kubadilishwa na wakati mwengine anamiss very important issues hazipot, mfano wakati wa mashindano ya mpira wa miguu Kombe na Miaka ya 50 ya Mapinduziit was very hot news lakini alikuwa haziweki kwa wakati na wakati mwengine hazikuwa up to date.
  Lakini Othman tumtafutie means za kuwa na wawakilishi crews na hata wapiga picha wasaidizi na waati mwenine hata hao watu wakumsaidia huko ofisini kwake ambako anaupload hizo data tunazomuomba, kwa nijuavyo mimi kwa sasa ni eke yake huyu na bado anasubiriwa na VP2 ofisi apige picha na adocument kwa wakati husika kwa maana hiyo anatumikia mwabwana wawili huyu na waswahili tunasema mwania mbili moja humpona. Tumtafutie wadhamini ambao watamuwezesha kuweza kuwaajiri watu wengi zaidi na wakati mwengine watakaomtumia hot news aweze kuwapa motisha. Hebu nawe Othman tupe mawazo yako kwa kujibu haya maoni yetu

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.