Katibu wa Jumuiya ya Kuhifadhi Mazingira Ras Fumba Ndg. Abdulrazak Shaban, akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya Utunzaji wa Mazingira kwa Wananchi wa Shehia sita za Dimani zilizoshiriki mafunzo hayo. ni Shehia ya Fumba, Bweleo, Dimani, Nyamanzi, Kombeni na Shakani. zimewakilishwa na Viongozi wa vikundi vya mazingira vya shehia zao.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Mazingira ya Ras Fumba na kufahiliwa na Mfuko wa Foundation for Civic Society.
Muwezeshaji wa Mafunzo ya Utunzaji wa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira Wilaya ya Magharibi. Ndg.Salim Ali Khamis, akitowa mafunzo ya Utunzaji wa mazingira na faida yake kwa Binaadam na Wanayama wanaoishi katika misitu mbalimbali ilioko Zanzibar. Amesema Misitu ina faida kubwa kwa Binaadamu katika maisha yake ya kila siku na misitu ihahitaji kuhifadhiwa.
Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo ya Utunzaji wa mazingira katika sehemu zao za makazi ili kuepusha madhara yanayotokana na uharibifu wa mazingira ya misitu, mafunzo hayo yamefanyika katika skuli ya msingi Bweleo Unguja Wilaya ya Magharibi.
Mshiriki wa Mafunzo hayo akichangia na kutowa mamawazo yake wakati wa mafunzo hayo ya Uhifadhi wa Mazingira Zanzibar wakati wa mafunzo hayo yalioandaliwa na Jumuiya ya Ras Fumba.
Mwananchi wa Kijiji cha Kisakasa akichangia katika mafunzo hayo na kueleza jinsi ya hali ya Kisakasa kulivyokuwa na uharibifu wa mazingira ya ukataji wa miti ovyo na kusababisha eneo hilo kuwa wazi tafauti na zamani eneo hilo lilikuwa likizungukwa na miti hata kukitokea upepo miti hiyo inakuwa kinga kwa maeneo ya Kijiji.
Muwezeshaji akijibu maswali yalioulizwa na wajumbe wa mkutano huo wa mafunzo ya utunzaji wa mazingira.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mazingira ya Ras Fumba Bi. Mary Shoka Hassan, akizungumza katika mafunzo hayo na kuelezea elimu hiyo wanayoipata waitumie kwa manufaa ya jamii na kutoa elimu kwa Wananchi.
No comments:
Post a Comment