Na
Joseph Ngilisho, ARUSHA
SHEIKH
wa msikiti wa Sawiyatu Qadiria,Hassan Bashiri (33) mkazi wa Tindigani,Unga Ltd
jijini hapa, amejeruhiwa vibaya kwa kumwagiwa tindikali na watu wasiofahamika
wakati akijerea nyumbani kwake usiku wa kuamkia leo.
Kwa
mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, tukio hilo
limetokea usiku wa kuamkia jana majira ya saa 3:45 usiku,ambapo Sheikh huyo
alikuwa akitokea mjini baada ya kuachana
na wenzake wawili waliokuwa wakijadili masuala ya kikao cha maulid.
Alisema
wakati akijerea nyumbani kwake alikutana na mtu mmoja aliyekuwa amesimama
kwenye kiambaza cha msikiti na kumsalimia, hata hivyo alisema hakumbuki iwapo alijibiwa, ila wakati
akiendelea kutembea alihisi kuna mtu anamfuata
kwa nyuma.
“Wakati
anaendelea kuelekea nyumbani kwake akahisi kuna mtu anamfuatilia na alipogeuka
ili ajue ni nani anamfuatilia ndipo mtu huyo alimwagia kemikali hicho kinachosadikiwa kuwa tindikali,”
alisema.
Alisema
mtu huyo baada ya kutimiza azma hiyo alitoweka kwa kutimua mbio na kuelekea
kusikojulikana,hata hivyo askari waliokuwa doria maeneo ya karibu walipata
taarifa na kuelekea eneo la tukio,ambapo walimkuta majeruhi huyo akiwa
hajitambui.
Kwa
mujibu wa Sabas polisi inamshikilia mtu mmoja kwa mahijiano kuhusiana na tukio
hilo,wakati huo huo majeruhi amelazwa hospitali ya mkoa Mount Meru kwa ajili ya
matibabu.
Matukio
ya viongozi wa dini kujeruhiwa kwa tindikali yamekuwa maarufu ambapo Asheikh
Saidi Makamba wa msikili wa Arumeru alijeruhiwa vibaya Julai 13 mwaka jana
kabla ya Katibu wa Bakwata, Abdulkarimu Jonjo kulipuliwa kwa bomu Oktoba 24,
2012.
Serekali na wapenda uzalendo wanapaswa kufanya upelelezi wa kina maana mji muhimu kama Arusha unakosa amani kwa sasa hasa kwa makasisi wa dini mbalimbali.
ReplyDelete