Habari za Punde

Balozi Seif Akutana na Meya wa Califonia na Kutembelea Ujenzi wa Hoteli Mpya Shangani Zanzibar.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Jimbo la California unaoongozwa na Meya wa Jimbo hilo Mstahiki Osby Davis aliyepo kulia yake.
Meya wa Jimbo la California Mstahiki Osby Davis  akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kuzungumza naye akiuongoza Ujumbe wa  Viongozi, Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Jimbo hilo kuangalia maeneo ya uwekezaji Nchini Tanzania.
Balozi Seif akiwa katika picha ya Pamoja na Ujumbe wa Jimbo la California Nchini Marekani uliopo nchini kwa ziara ya siku tatu kuangalia fursa za uwekezaji Vitega Uchumi.kulia ya Balozi Seif ni Meya wa Jimbo la California Mstahiki Osby Davis na Mjumbe wa Sakramento ya Jimbo hilo Bwana Shabir Jiwa.Kushoto ya Balozi Seif ni Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Zanzibar ambaye ndie mwenyeji wa Ujumbe huo Bwana Ali Aboud pamoja na Mjumbe wa Sakramento ya Jimbo hilo Bibi Wanjiru Wanjiru.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar Nd. Issa Sarboko Makarani akimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Juhudi zilizochukuliwa na Kampuni ya ASB Holdings za ujenzi wa Hoteli ya Daraja la Saba Shangani uliozingatia mpango wa Umoja wa Mtaifa ya Uhifadhi wa Mji Mkongwe.Kulia ya Balozi ni Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Nd. Ali Khalil Mirza. 
Picha no:-857 ni:- Balozi Seif akiangalia mandhari nzuri wa Bahari ya Hindi akiwa juu ya Hoteli ya Daraja la Saba iliyopo Shangani Mjini Zanzibar wakati alipokuwa akikagua maendeleo ya ujenzi wa Hoteli hiyo.
Moja kati ya vyumba vilivyomo ndani ya Hoteli ya Daraja la Saba iliyopo Shangani Mjini Zanzibar ambayo inaendelea na ujenzi wake ikiwa katika hatua za mwisho mwisho.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.