Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibanda maiti Zanzibar,
Mjumbe wa kamati ya maridhiano, Mansoor Yussuf Himid (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Habari na Haki za Binadamu wa CUF Salim Bimani, kwenye mkutano wa hadhara wa CUF uliofanyika Kibanda maiti.
Wafuasi na wapenzi wa CUF wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibanda maiti.
Wafuasi na wapenzi wa CUF wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya kibanda maiti.
Picha na Salmin Said, OMKR
Na Khamis Haji, OMKR
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema hakufurahishwa na baadhi ya kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete alipokuwa akizindua Bunge Maalum la Katiba na ameamua kumwandikia barua kumueleza masikitiko yake.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulioandaliwa na Chama cha CUF katika viwanja vya Kibandamaiti, Mhe. Maalim Seif alisema, Rais Kikwete kama mkuu wa nchi, hakupaswa kuingiza misimamo ya chama chake kwa vile Katiba inayoandikwa ni ya wananchi wote na sio wa chama maalum.
Maalim Seif alisema Rais alitarajiwa angetoa hotuba ambayo inawanunganisha Watanzania wote, lakini kilichotokea alitoa kauli ambazo ni za ubaguzi ambazo ni za kujenga chuki dhidi ya watu fulani.
Alisema kwa mfano Rais kueleza kuwa wananchi wa Pemba ndio watakaoathirika chini ya mfumo wa Serikali tatu kwa vile ndio wenye mashamba mengi ya Vitunguu katika maeneo ya Tanzania Bara ni kauli ya kujenga chuki, kwa vile sio watu kutoka Zanzibar peke yao wanaofanya shughuli zao Tanzania Bara.
“Sikutarajia hata siku moja Rais Kikwete atafitinisha watu, … eti Wapemba watafukuzwa, lakini Tanzania Bara wapo Wakenya na hata Wachina wanafanya shughuli zao, kwanini iwe Wapemba tu”, alihoji Maalim Seif.
Alisema baada ya hotuba hiyo ya Rais, na nia ya CCM kulazimisha mfumo wa serikali mbili, licha ya wananchi wengi kupinga, msimamo wake yeye na Wazanzibari walio wengi sasa unabaki kuwa ni Serikali ya Mkataba, kama walivyotaka kwenye maoni yao kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Makamu wa Kwanza wa Rais ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF, alisema ishara za kuwa CCM hakina nia ya wananchi kupata katiba safi na kulazimisha misimamo yao inaonekana wazi katika uendeshaji wa Bunge la Katiba.
Alisema Mwenyekiti wa Bunge hilo kwa kushirikiana na wajumbe wa CCM wamekuwa wakitumia wingi wao kulazimisha hoja zao, pamoja na kuteua viongozi kutoka chama hicho ili kupitisha matakwa yao, hata kama hayana maslahi kwa wananchi walio wengi.
Alieleza kuwa hata Tume zilizioundwa na Mwenyekiti Samuel Sitta ni za upendeleo ambao takriban wajumbe wote ni kutoka CCM.
“Wenyevitio wote ni kutoka CCM anayewakilisha makundi mengine ni Hamad Rashid, sita akamteua Profesa Lipumba aingie, Mnyamwezi yule yuko makini amekataa, tunampongeza sana Profesa Lipumba”, alisema.
Aidha, alimpongeza Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe, Pandu Ameir Kificho kutokana na ujasiri na uwezo mkubwa aliouonesha alipokuwa Mwenyekiti wa muda wa Bunge Maalum kwa kufanya kazi bila upendeleo.
Maalim Seif alisema Mhe. Kificho alifanya kazi kubwa nzuri tena bila ya kuwa na kanuni, lakini Mwenyekiti Sitta ameonyesha udhaifu mkubwa wa kuendesha Bunge hilo.
Mfa maji ,haachi kutapatapa.
ReplyDeleteMaalim Seif ulipokuwa mtoto mzuri kwa Nyerere,ile siku Nyerere alipotaja ,chini ya kivuli cha muungano hakuna ubaguzi lakini ukivunjika kutakuwa na Wapemba na Wanguja,wabara na wa zanizibari na wazanzibara,jee kwa kuutaja Upemba ulimuandikia barua wewe. Wacha unafiki wewekama huna la kufanya sio kumuandikia barua ,bora kashughulikie madawa ya kulevya ndo kazi uliopangiwa..
ReplyDeleteacheni maneno yenu ya kipuuzi anony 1 and 2 , angalieni manufaa kwa wazanzibari kwanza , maneno aliyozungumza sefu sharif ni murua, kama ni muungano basi wa mkataba vinginevyo hatutaki kabisaaa huo muungano wanatulazimisha tu , acheni kufikiria manufaa ya kibinafsi ndugu zangu muwe na uchungu na visiwa wvyetu vio njiani kumalizwa kabisa na hii katiba ya lala salama
ReplyDeleteKujitoa katika kamati yule Mnyamwezi hivi sasa si ujasiri,ni udhaifu mkubwa mbele ya Taifa letu.Huoo ni wakati wa kupigania kupatikana kwa katiba mpya na ameonekana yeye anafaa kuwa kiongozi wa kuwa mstari wa mbele kuongoza mapambano haya,sasa anapojitoa katika mapambano si ujasiri ni sawasawa na mpiganaji mwoga ni sawasawqa na mpiganaji asemae "najitoa ,kama mnaweza piganeni peke yenu mie siye." Hapahitajiki nongwa hivi sasa panahitajika ujasiri na ushupavu.Maalim usimsifu bure mnyamwezi yule kwa tendo hilo na ujuwe ameshapoteza credibility na profile lake mbele ya jamii kwa sasa bure ghali,ghali bure. Si umemsifu mwanafunzi wako Kificho ,Y? kwasababu amehimili .
ReplyDeleteacheni longolongo, itoweni Tanganyika kwenye koti la muungano kama mnataka udugu wa kweli...
Deletemaalim sefu wewe ni mwalimu.Lazima ujuwe utafauti kati ya maneno yafuatayo.KUKEMEA,KUSHAURI,na KUWASA. Kitwete katika hotuba yake amewaasa na kuwashauri wabunge juu ya hatari za baadae kama itakuwa hivi au vile. Na katoa mfano tu ili aelewekee zaidi kama wewe pale ulipokuwa mwalimu ulipokuwa darasani kwako ukitoa mifano kadhaa ili wanafunzi wako wakielewe nini ulichokifahamisha. Mimi ni mpemba menyu na sioni sababu kwanini panganganiwe hilo linalo nganganiwa na wazanzibari.Maana siku tayari asset zangu nilizozichuma mika nenda miaka rudi zisizo hamishika tangu Muheza, Dar hadi Ntwara leo zijenkuwa ngawira.Utaratibu wa sasa nauwafiki na sioni kama kuna haja ya kuubadili madam una usalama amani na ushirikano kwa ndugu wa pande zote mbili za muungano huu.
ReplyDeleteww number mbili una matitizo na una chuki zimekujaa mm kikwete namuunga mkono kwa mambo mengi lkn kwa hutuba ile ni hutuba yake haifai imejaa vitisho na imelifanya bunge kuwa gumu sana na sifikirii kama kuna katiba ya wananchi itakayopatikana
ReplyDeleteHuyu,mh mansuri ni cuf kama wahadimu walivyo mtuhumu auvipi?
ReplyDeletemm sina mengi ila nakuombea uzima na umri maalim seif mungu akupe uwezo kuendelea kuitetea nchi yetu mpaka tupate uhuru kamili , usikubali kurudi nyuma wala usikubali kuchukua rushwa ili uziuze haki zetu. ZANZIBAR KWANZA
ReplyDeletendugu mpemba anon 6 usiwe na wasiwasi hizo mali zako hazigusi mtu kama watu wanaelewa tunachozungumza, labda nikuulize kwani kule tanganyika hakuna watu wa mataifa mbali mbali wamewekeza kama kutoka amerika, ulaya , uturuki , ujapani na uchina nk? jee wao na nchi zao zina muungano na tanzania ? sasa unapaparika nini ndugu yangu sisi tunataka uhuru wetu , mimi si mpemba ila muunguja halisi nasema hivi , na nina mali zangu na biashara zangu arusha na mwanza
ReplyDeleteKatika taifa letu hili la Tanzania au Zanzibar inategemea msomaji uko upande gani wa nchi hizi kuna dini mbili kwa nne,uislamu.ukristo,ubaniani na Uccm.
ReplyDeletehapa Tanzania CCM ni dini hili itabidi tukitaka tusitake tukubali kwani misahafu na bibliani vyote vimekiukwa kwa wakati tofauti ili kukidhi haja ya katiba ya chama hiki.
mimi sio muumini wa chama cha siasa nikisema sio muumini nina maana siabudu chama haina maana sina chama ninacho na sifuati yale yanayohubiriwa na maaskofu au masheikh wa chama changu ikiwa naona hayana maana kwa taifa langu au kwa jamii ninayoishi kwa wakati huu na huo unaokuja.
sasa ikiwa tuna sikiliza maagizo ya viongozi hasa wa ccm halafu wajibu wetu watanzania ni kufuata maagizo hayo kama mbuzi au kondoo wanavyomfuata mchungaji iko haja ya sisi watanzania au wazanzibari badala ya kutilia mkazo kwenda kupima ukimwi au malaria mahospitalini basi sasa wakati umefika wa kwenda kupima vichwa vyetu sote.
tukajua nani amewahi kuugua wazimu na nani ana wazimu wa kuzaliwa nao kwani kusema sote tuna akili timamu hilo itakuwa tunafanya kosa.
katiba ya wananchi wa taifa hili iwe Zanzibar au Tanzania ambayo ni Tanganyika ni bora niseme wazi kwani Tanzania ni Tanganyika na Zanzibar ni unguja na Pemba.
kwa nini iwe lazima ipate Baraka ya chama cha siasa kimoja ambacho ni ccm wengine kwa kuitwa wapinzani haina maana kuwa hawaitakii mema nchi hii au hawana haki ya kushiriki katika kutafuta katiba haki ya kutengeneza katiba mpya ili ikidhi matakwa ya ccm nani kawapa haki hiyo peke yao?
ni vigumu kuwa na chama kilichozowea kuwa pekee cha siasa bila mpinzani halafu baada ya mageuzi ya vyama vingi bado wana fanya shughuli zao kama vile vyama vingine ni vilabu vya kunywa pombe.
matatizo yatatukuta hapa zanzibar au Tanzania ikiwa hatutokuwa makini na kulishughulikia hili tatizo sugu katiba haitopatikana na ikipita huko Dodoma ya ccm kwa wananchi haitopita sasa suala la kujiuliza hizi pesa za walipa kodi zinazoliwa bure kwa kisingizio cha katiba isiyokubalika kwa wananchi zinawauma wananchi au la?
ni wazi wanaokula haziwaumi.
ccm wanatarajia kupitisha kwa mabavu katiba hii kwa wananchi baada ya kuipitisha hapo Dodoma kwa kuwa wao ndio wengi humo bungeni hili si la kustaajabu kwa sababu aliewachagua ni mwenyekiti wao na wasaidizi wake.
mimi napenda haki itendeke hata kama inaniuma au itaninyima mimi binafsi raha lakini ikiwa ni haki ni vema ikatendeka sasa la kujiuliza viongozi wetu hapa Zanzibar wanaipenda au wana taka haki itendeka hata kama itawanyima usingizi?
dalili zinaonyesha wote wanaona bora walale usingizi mzito wa kukoroma hata kama itawagharimu nchi yao ya Zanzibar kuwa mkoa ili muradi wao waendelea kupanda magari yenye vingora na kupokea mishahara minono huku wananchi wao wote wakipita wakiomba omba mitaani na madukani.
mungu tunusuru na viumbe wako waliokithiri kiburi cha mauti na utuondolee maradhi,njaa,,fitna ya wenyewe kwa wenyewe na watu baki na kutuepesha na hili kaburi refu tunalojichimbia wenyewe huko Dodoma hivi sasa.
ameen.
mzaliwa visiwani unguja na Pemba yake.
Zanzibar.
Ehhh jamani nyee "kuna shimo huko msiende ,bora pitine huku",ikachukuliwa huyu jamaa kalazima huku tusipite! hiyo ni tafsiri tuu.Lakini kiujumla ametuasa,na kama tukipita likitoa lisilo jema,itachukuliwa vipi,kakhini kusema au vipi.Muungwana anapoona huku kuna hatari na akatoa indhari ni wajibu wake jamani !!!!.
ReplyDeleteWaswahil wanasema mtoto akililia wembe mpe sasa kwann nyie muna unga ngania wapen wazanzibar nchi ikiwashinda kimpango wao muki ngangania mutaonesha picha mbaya mpaka kwetu ss vijana tusokuwa na maendeleo miaka nenda miaka rudi mimi haya nimaoni yangu km mtanzania masikin ila naipenda znz sana na sina ubaguzi kati ya pemba na unguja na hata bara kwan mimi baba mpemba mama muunguja mkewangu mbara na watoto wangu nimezaa bara
ReplyDelete