Na Mwandishi Wetu.
JESHI
la Polisi Zanzibar linaendelea kuwasaka watu waliohusika katika miripuko ya
mabomu yaliyotokea hivi karibuni pamoja na majambazi yaliyomuua askari polisi
Koplo, Mohammed Mjombo.
Mkurugenzi
Msaidizi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Zanzibar,Yussuf Ilembo, alisema hadi
sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliekamatwa katika matukio yote mawili.
Miripuko
ya mabomu yalitokea katika makanisa
mawili likiwemo la Mkunazini na mkahawa wa Mercury uliopo Malindi.
Aidha
tukio la ujambazi lilitokea katika hoteli ya Pongwe Bay Resort, ambapo
majambazi hayo mbali ya kumuua Koplo Mjombo pia yalimjeruhi, PC Ibrahim Juma
anaeendelea kupatiwa matibabu na kumpora silaha yake aina ya SMG ikiwa na risasi 30.
Aidha
alisema bunduki iliyoporwa na majambazi hayo pia haijapatikana ingawa juhudi za
kuitafuta zinaendelea.
“Hadi sasa
bado hatujakamata watuhumiwa katika matukio hayo lakini tunaendelea na
upelelezi,” alisema.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya matukio ya mabomu, Kamishna wa polisi Zanzibar,
Hamdan Omar Makame, alisema mabomu yaliotumika katika matukio hayo ni ya
kienyeji na upepelezi ulikuwa ukifanywa kwa kusaidiana na makachezo kutoka
makao makuu ya polisi Dares Salaam.
Pia
alisema miripuko hiyo ilikuwa haihusiani na masuala ya dini, siasa au shughuli
za kitalii.
No comments:
Post a Comment