Na
Lorietha Laurence, MAELEZO
WAZIRI
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid, amesema asilimia 1.03 ya vifo
hutokana na ugonjwa wa figo.
Alisema
hayo wakati akitoa tamko kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, kuhusu
siku ya afya ya figo itakayoadhimishwa Machi 13 mwaka huu mjini Dodoma.
Kauli
mbiu ya maadhimisho hayo ‘figo huzeeka, kadiri mtu anavyozeeka. Jali afya ya figo
zako.’
Hivyo
aliwataka Watanzania kuchukua hatadhari kujikinga na ugonjwa huo mbaya.
“Nawasihi
watu wawe na taratibu za kufanya vipimo mara kwa mara, pia kujali afya zao kwa
kuwekeza katika maendeleo ya afya zao ili kujikinga na ugonjwa wa figo,”
alisema.
Aliongeza
kuwa ugonjwa huo husababishwa na shinikizo la damu, ugonjwa wa kisukari na
kutokufanya mazoezi mara kwa mara,msongo wa mawazo,unywaji pombe, unene uliokidhiri,ulaji usiofaa,
matumizi ya chumvi na mafuta pamoja na uvutaji sigara.
Alisema
ugonjwa huo unaweza kumuathiri mtu yeyote aliye katika umri wowote, ingawa
hujitokeza zaidi kwa watu wenye umri wa miaka 50, ambapo takwimu zinaonesha
kati ya mwanamme mmoja kati ya watano na mwanamke mmoja kati ya wanne wenye
umri wa miaka 65 hadi 74 wana ugonjwa wa figo.
Alisema
figo ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu, husaidia kuchuja na kuondoa
taka mwilini, majimaji yaliyozidi na
kudhibiti kiwango cha kemikali mwilini kwa kudhibiti shinikizo la damu.
Aliwataka watu waepukane na ugonjwa huo kwa kufuata
ushauri wa wataalamu na kuzingatia
mazoezi, kunywa glasi 6 hadi 8 za maji
kwa siku,kuepuka matumizi ya sigara na bidhaa zinazotokana na tumbaku,
kuzingatia maelekezo ya wataalamu, kutumia dawa kwa usahihi na kufuatilia kiwango
cha sukari mwilini.
Maadhimisho
ya afya ya figo duniani yalianza mwaka 2006, ambapo mwaka huu yataadhimishwa
kuanzia Machi 10 hadi 14 Machi, katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mjini
Dodoma, shughuli zitakazofanyika ni pamoja na kutoa huduma ya kupima afya ya
figo.
No comments:
Post a Comment