Habari za Punde

Rais Kikwete akiwa kazini ndani ya Ndege kuelekea Dodoma.

Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa  ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma  huku  akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la  ya Kanuni za Bunge Maalum. Picha na Ikulu.U


1 comment:

  1. ndugu mwandishi unasahau mamilioni ya fedha za wakulima na wafanyakazi zilizotumika kununua hii ndege ? kweli kulikuwa na ulazima wa kununua ndege ya rais? kwani sisi tumejitosheleza kiasi hicho? tunapenda kuiga tu basi bila kufikiri

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.