Wasani walipokuwa wakilishambulia jukwaa katika tamasha la Shtuka Sasa lililofanyika viwanja vya kibanda maiyi Zanzibar.

Tamasha
la ‘Shtuka Sasa’ la Zantel lapongezwa na wananchi Zanzibar
Idadi kubwa ya wananchi
waliohudhuria tamasha la wazi la ‘Shtuka Sasa’ lililoandaliwa na kampuni ya
simu za mikononi ya Zantel mwishoni mwa wiki hii wameipongeza kampuni hiyo kwa
kuwaletea burudani hiyo visiwani hapa.
Tamasha hilo lililofanyika
katika Uwanja wa Kiembe Samaki lilihudhuriwa na maelfu ya wakazi wa kisiwani
humo ambao waliimba na kucheza na wasanii hao, liliandaliwa ili kuwapa fursa
wateja wa Zantel kujifunza zaidi kuhusu huduma za kampuni hiyo.
Likitumbuizwa na wasanii
wakali wa muziki wa kizazi kipya kama Chege,
Madee, Dogo Asley, tamasha la Shtuka Sasa, lilifanikiwa kukonga nyonyo za
wakazi wa Zanzibar kwa kiasi kikubwa.
Akizungumza wakati wa tamasha
hilo, Afsa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan alisema tamasha hilo ni
mfululizo wa mengine yatakayofanyika nchi nzima ili kuwapa fursa wateja wao
kuzitambua zaidi huduma za Zantel na kuzifurahia.
‘Toka mwaka huu uanze, Zantel
imejikita kwenye kuwaelimisha wateja kuhusu ubora wa huduma zetu kupitia
matamasha, ambayo yatafanyika nchi nzima’ alisema Khan.
Tamasha la Zanzibar
lilifunguliwa na wasanii wa kikundi cha B-Six wakifuatiwa na msanii Sultan King
ambaye ni mmoja wa wasanii wanotamba sana kisiwani Zanzibar kwa sasa.
Wasanii wengine waliopokewa
kwa shangwe kubwa ni Dogo Aslay na bendi yake ya Mkubwa na Wanawe ambao waliimba nyimbo zao kali kama ‘Mapenzi
ya Kitoto’ na nyingine nyingi.
Baadhi ya wananchi
waliohudhuria tamasha hilo wameipongeza kampuni ya Zantel kwa kuwaandalia burudani
hiyo kisiwani hapo.
‘Kama kampuni inayoongoza
kisiwani hapa tunaishukuru Zantel kwa kutuletea burudani nzuri ambayo pia
imetupa fursa ya kujifunza zaidi kuhusiana na huduma zinazotolewa na kampuni
yetu kama Mpaka Basi na nyinginezo’ alisema Ashfa Mohamed, mmoja ya mashabiki
waliohudhuria tamasha hilo.
Pia ikiwa ni mwendelezo wa
kampeni yake kuhamasisha wateja wao kusajili laini za simu, Zantel pia ilitumia
tamasha hilo kusajili laini za wateja wao kupitia mabanda yaliyosambazwa uwanja
mzima.
No comments:
Post a Comment