Na
Mwandishi wetu
MWENYEKITI
wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, leo anatarajiwa kwenda
bungeni kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba kwa wajumbe wa bunge hilo .
Mwishoni
mwa wiki iliyopita, Mwenyekiti wa bunge, hilo Samuel Sitta, aliwambia wajumbe
kuwa Jai Warioba atakaribishwa leo kuwasilisha rasimu hiyo kwa mara ya kwanza
kwa bunge hilo .
Baada
ya Jaji Warioba kuwasilisha rasimu, itakuwa zamu ya Rais Jakaya Kikwete
kulihutubia bunge hilo Jumanne au Jumatano, kabla ya kazi ya kuchambua na
kujadili kifungu kimoja baada ya chengine kuanza.
Hata
hivyo, kwa mujibu wa kanuni za bunge hilo, Rais alipaswa kutangulia kulihutubia
bunge hilo
kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Mjumbe
wa bunge hilo, ambae alishiriki kazi ya utungaji rasimu, Tundu Lissu, wiki
iliyopita alimtikiza Mwenyekiti wa bunge, akisema amevunja kanuni kwa
kuwatangazia wajumbe kuwa Jaji Warioba atakaribishwa Jumatatu wakati rasimu
inataka Rais atangulie kwanza.
Akiomba
mwongozo, Lissu alisema kanuni inamtaka Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge
kwanza kabla ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
kuwasilisha rasimu ya katiba bungeni.
“Mwenyekiti
naomba mwongozo wako kuhusu tangazo lako kwamba Jaji Warioba atakuja
kuwasilisha rasimu yake ndipo Rais aje kulihutubia Bunge, kanuni zetu zinamtaka
Rais aje kwanza kulihutubia Bunge ndipo Jaji Warioba aje kuwasilisha rasimu
yake.”
“Tuliamua hivi kwa kuwa tuliona iwapo Jaji Warioba akitangulia
kuwasilisha rasimu baada ya hapo ndipo Rais aje kulihutubia Bunge itaonekana
kama Rais Kikwete amekuja kumjibu Mwenyekiti wa Tume,” alisema.
Alisema
kwa mujibu wa kanuni hizo, kazi ya kwanza inayotakiwa kufanywa na wajumbe
inaanzia katika kamati zitakazoundwa na kuhoji Sitta ametumia kanuni ipi
kuruhusu mjadala wa siku tatu.
Akijibu
hoja hizo ya Lissu, Sitta alisema Rais hawezi kuja kulihutubia Bunge wakati
hakuna ajenda yoyote iliyowasilishwa kwa wajumbe.
“Kwa
uzoefu wangu katika bunge lazima kwanza tuwe na ajenda, Jaji Warioba atakuja
kuwasilisha rasimu ili tuwe na ajenda mkononi ndipo Rais aje kulihutubia Bunge.
Tumelijadili hili na wenzangu tumeona iwe hivyo ikiwezekana tutatengua kanuni
kumruhusu Jaji Warioba kuwasilisha kwanza rasimu ya katiba kwa wajumbe,”
alisema
Alisema
kanuni zinamruhusu kutumia busara yake kuamua baadhi ya mambo kwa namna anavyoona
inafaa hivyo ametumia madaraka yake kuamua hivyo ili wajumbe wawe na mjadala
mpana kabla ya kwenda kwenye kamati.
“Katika
kipindi hiki pia nitapata muda wa kuwajua wabunge na hivyo kuweza kuwapanga
katika kamati mbalimbali, wajumbe zaidi ya 600 mliopo humu ni wengi lazima
nipate muda wa kutafakari kabla ya kuunda kamati,” alisema.

nasikia kuna wajumbe kupigwa msasa kuhusu historia ya mapinduzi na muungano nk , ikiwa wajumbe watanganyika hawajui hilo ni tatizo lao , onyo kwa wajumbe wa zanzibar msikubali kuleweshwa na maneno yoyote yale sisi tunataka uhuru wetu tu! asije kikwete wala nani kukwambieni chochote , mshikamane kuwa kitu kimoja mudai uhuru wetu , historia na mengineyo tunayajua sisi ukweliwake sio historia inayoandikwa vitabuni ,
ReplyDelete