Na Rose
chapewa, Mbeya
MAUAJI ya vikongwe,
albino, rushwa na kujichukulia sheria mkononi, ni moja ya mambo yaliyosababisha
nafasi ya Tanzania
katika masuala ya utawala bora kushuka.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais na Utawala Bora, George Mkuchika, alisema hayo wakati
akifungua mkutano wa wa kamati ya
ushauri ya mkoa jijini Mbeya (RCC), na
kuseoma tabia ya wananchi kujuchukulia sheria mkononi imechangia kwa kiasi
kikubwa Tanzania
kushuka kwenye sualala utawala bora.
Alisema
katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mikoa ya Shinyanga, Simiyu Mwanza na
Mbeya kumekuwa na mauaji yakiwemo ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino).
Alisema
pamoja na mauaji hayo, wananachi wamekuwa wakijichukulia sheria mkononi, hali ambayo inachangia kwa kiasi
kiukubwa Tanzania kufanya vibaya katika
utawala bora na kushika nafasi ya 70 kati ya mataifa 170 yaliyofanyiwa utafiti
kuhusu utawala bora.
Aidha Waziri
huyo pia alizungumzia Suala la mapambano dhidi ya rushwa
ambalo alisema ni miongoni mwa
viashiria vya utawala bora vinavyochukuliwa na mataifa mbalimbali duniani.
Akizungumzia
rushwa, alisema imesababisha madhara
mengi kwa jamii pamoja na misingi ya utawala bora, na kwamba madhara hayo
yanaweza kuhatarisha uhai na usalama wa taifa.
Waziri
Mkuchika alizitaja athari zitokanazo na rushwa
kuwa ni pamoja na kutotimiza utekelezaji wa majukumu ya serikali,
kukwamisha utoaji wa haki na kuongezeka kwa maovu katika jamii.
Madhara
mengine ni wananachi kukosa imani na serikali yao na kujichukulia sheria
mkononi, kukosekana huduma muhimu za kijamii, kutolewa huduma duni, kuwa na
viongozi wasio waadilifu, kusababisha kupungua kwa pato la serikali na hivyo kupunguza
uwezo wa serikali katika kuhudumia wananchi.
No comments:
Post a Comment