Waandishi wakiwasili Kijiji kwa Maangwi Kiongoni Shegejuu wilaya ya Wete , kulia Juma Mmanga , Mwarab Mmadi (StarsTV)
Wandishi wakisalimiana na Shekh Masoud Sanani walipowasili Kijijini kwao
Shekh. Masoud Sanani akizungumza na waandishin waliofika kumtembelea kujua hali yake, wakati akipata matibabu, kijiji kwao Maangwi Kisongoni Shegejuu Wilaya ya Wete Pemba, aliyesimama ni Ndg. Juma Mmanga.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Shekh. Masoud akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbalin waliofika kumuangalia.
Waandishi wa vyombo mbalimbali waliofika Pemba kwa kutembelea miradi ya Maendeleo kisiwani humo, ikiwa na timu ya Waandishi kutoka Dar-es-Salaam na Zanzibar. walifika kumjulia hali mwandhishi mwezao wa Gazeti la Mwananchi akiwa ni Mhariri wa Habari za Michezo Ndg. Masoud Sanani.
Mwakilishi wa Wandishi Juma Mmanga akimkabidhi mchango wa papo kwa papo uliochangwa na waandishi hao wakati walipofika kumtembelea Ndg. Masoud Sanani, kijijini kwao Pemba
Ndg. Juma Mmanga akitowa shukranin kwa niaba ya waandishi waliofika kumuagalia mwandishi wa Gazeti la Mwananchi Mhariri Mkuu wa michezo Ndg. Masoud Sanani.
Shekh. Juma Mmanga akisoma dua kumuombea Ndg Masoud Sanani, kupata nafuu na maradhi yake na waandishi wate waliofika kumtembelea.
Ndg. Masoud Sanani akitowa shukrani kwa Waandishi waliofika kumuagalia na kumtakia afya njema, amewashukuru na kuwatakia kazi njema, na kufarijika na ujio wao kumtembelea na kujua hali yake, na kusema anaendelea vizuri na hali yake ni nzuri akiendelea na matibabu.
Waandishi wakiwa kijijini kwa Ngd Masoud Sanani ealipofika kumtembeleac na kujua hali yake.
Waandishi wa habari wakiwa na Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Mwananchi Ndg. Masoud Sanani mwenye kazi, walipofika kijijini kwao katika kijiji cha Maangwi Kiongoni Shegejuu wilaya ya Wete,kumjulia hali yake, wakati wakiwa katika ziara kisiwani humo.
Waandishi wa habari wa Vyombo mbalimbali vya habari wakiwa katika picha ya pamoja na Mhariri wa Michezo wa Gazeti la Mwananchi Ndg. Masoud Sanani.walipofika kumjulia hali.
Habari ingekuwa nzuri zaidi kama ingeambatana na maelezo japo kidogo, bila maelezo inakuwa vigumu kupata undani wa hizi picha, mfano jee huyu mwandishi mwandamizi ni mgonjwa, amestaafu au vipi? Picha imepigwa kijijigani huko Pemba? na majina ya waandishi waliomtembelea sio wote tunaowajua ukiondoa Munir Zakaria
ReplyDeleteHongera ndugu Othman kwa kufuata ushauri wa hapo juu. Unaona utamu wa habari huo sasa, tumepata kumjua Juma Mmanga, Massoud Sanani pamoja na kijiji anachotoka. Habari iko wazi na inafahamika kwa kiasi chake. Shukraaaaaaan
ReplyDelete