Na Matrida Mwenzegule
Wakati Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter
Muhongo, akitanganza kiama kwa wazee na wasio na elimu za kutosha wizarani
kwake, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), Hawa Ghasia, ametangaza kifo cha walarushwa kupunguza kero wizarani
kwake.
Katika
hotuba yake kwa wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo mjini hapa, Ghasia
alimwagiza katibu Mkuu wa wilala hiyo,
Jumanne Sagini, kuanza mchakato wa
kuwatambua watumishi wote wanaotuhumiwa kwa rushwa na kuhujumu mamlaka za serikali kwa masilahi binafsi.
Katika
baraza hilo lililokutana kwa lengo la kuboresha utendaji na uwajibikaji, Ghasia
pia aliwataka wafanyakazi kuacha kulalamika badala ya kuwajibika.
Alisema
wizara imegeuka jaa la malalamiko dhidi ya wizara zikiwemo kero mbalimbali za
rushwa, watumishi wabovu kubebwa bila tija, uwajibikaji mbovu hasa katika kuwatendea haki watumishi jambo
linalochangia kurudisha nyuma
maendeleo.
Aliwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kutumia mabaraza ya wafanyakazi kujadili mambo mbalimbali yanayohusu masilahi na ustawi
wa wafanyakazi na kuishauri manejimenti
ya utumishi ili waweze kutekeleza majukumu yao.
Alilitaka
baraza hilo pia
kujadili namna rasilimali zinavyotumika
vibaya kwa maslahi ya wachache.
Alisema wakitumia mabaraza hayo vizuri malalamiko
ya wafanyakazi katika wizara hiyo yatapungua na kuongeza uwajibikaji wa kazi katika wizara hiyo.
No comments:
Post a Comment