Habari za Punde

Maalim Seif afungua mkutano mkuu wa CUF Wilaya ya magharibi

  Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho mzee Machano Khamis Ali kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa uchaguzi (CUF) Wilaya ya Magharibi Kilimahewa.
Baadhi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Wilaya ya Magharibi (CUF), wakisikiliza maelekezo juu ya namna ya kuwapata viongozi bora. (Picha na Salmin Said, OMKR)

Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim  Seif, ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF, amefungua mkutano mkuu wa uchaguzi (CUF) Wilaya ya Magharibi Unguja, na kuwasisitiza wajumbe wa mkutano hao kuchagua viongozi watakao kuwa tayari kukitumikia chama hicho.

 Amesema wajumbe hao wana jukumu kubwa la kuchagua viongozi majasiri, wenye busara na hekima, na wasioweza kurubiniwa na hatimaye kukisaliti chama kwa maslahi binafsi.
 
Katika mkutano huo uliofanyika ofisi za CUF Wilaya ya Magharibi zilizopo Kilimahewa Zanzibar, Maalim Seif pia aliwanasihi wajumbe hao kuepuka makundi na vitendo vya rushwa katika kupata viongozi bora.
 
Mkutano huo wa uchaguzi ni mfululizo wa mikutano ya uchaguzi ndani ya chama hicho katika ngazi za Wilaya, ambapo Wilaya za Zanzibar zinatarajia kukamilisha chaguzi hizo mwishoni mwa wiki hii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.