Habari za Punde

Mdahalo wa Katiba Mpya

Muungano wa Asasi za Kiraia Tanzania umeandaa Mdahalo wa wazi  kuhusu
 Changamoto za Mchakato wa Katiba Mpya.

Mdahalo huo utafanyika tarehe 31/5/2014 katika Ukumbi wa Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza, jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8.00 mchana hadi saa 10.00 jioni.

Mdahalo huo utatangazwa mojakwa moja na vituo vya ITV, ABM Radio ya Dodoma, pamoja na
Chuchu FM na Istiqama Radio za Zanzibar.

Vyombo vingine vya habari vitakavyopenda kuutangaza mdahalo huu wa maslahi ya umma pia vinakaribishwa.

Watoa Mada ni waliokuwa Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba: Prof. Mwesiga Baregu na Bw. Awadhi Ally Saidi.

Wananchi wote mnakaribishwa kushiriki katika mdahalo huu ili kuhakikisha kuwa Tanzania inapata katiba
mpya inayokidhi maslahi yaWatanzania.
Nyote Mnakaribishwa!

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.