Waziri wa Uwezeshaji Zanzibar na wa Jimbo la Makunduchi, Mhe Haroun Ali Suleiman akiwa katika ukumbi wa baraza la Wawakilishi akifuatilia michango ya Wajumbe wakichangia Afisi ya Rais, katika kipicha cha michango asubuhi na jioni yake kupitishwa Bajeti hiyo.
Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Zanzibar Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Mhe, Makame Mshinba, wakati wa michango ya Bajeti ya Afisi ya Rais, ikichangiwa na wajumbe katika ukumbi huo.
Maafisa wa Afisi ya Rais wakifuatilia michango ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakichangia Afisi yao, wakati wa michango.
Mwakilishi wa Jimbo la Chumbuni Mhe Machano Othman, akisalimiana na Afisa Mkuu wa Sensa Zanzibar Ndg Mohammed Hafidh.baada ya kuahirishwa kikako cha asubuhi. 
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Mhe Salmin Awadh, kulia akizungumza na Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum, wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano.
Mhe.Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Dkt. Mwinyihaji Makame, akizungumza na Katibu Mkuu wake Ndg. Salum Maulid, baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi kwa ajili ya mapumziko ya mchana.
Naibu Katibu wa Rais Mhe. Maryam Mrisho akimpongeza Mhe Waziri Nchi Ofisi ya Rais Mhe.Dkt. Mwinyihaji Makame, baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi wakati wa kuwasilishwa michango ya wajumbe wa Baraza.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe. Salum Maulid akimfafanilia jambo Mwakilishi wa Jimbo la Kwahani Mhe Ali Salum, wakiwa nje ya Ukumbi wa Baraza baada ya kuahirishwa kwa kikao cha asubuhi kwa mapumziko, ilikurejea jioni kuendelea na michango ya Ofisi hiyo na kupitisha Bajeti yake.
No comments:
Post a Comment