Habari za Punde

Ziara ya Mbunge wa Kikwajuni ZAWA.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Ndg. Mustafa Ali Garu, akizungumza na Ujumbe Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar, Mhe.Hamad  Masauni, alipofika ZAWA Mabluu, kuzungumzia Mrasi mkubwa wa Maji katika Jimbo la Kikwajuni unaoendelea na taratibu zake ukiwa katika hatua za mwisho kumalizika baada ya kukamilika kwa uchimbaji wa Kisima Kaburikikombe.
Mhe. Hamad Masauni akiwa na ujumbe wake na Mkurugenzi wa Taasisi ya The Registered Trustees of Communication for Development Africa Initiative, Ndg. Gaston Modest Kaziri,Mkujumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Kikwajuni Mbeto, wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaya ya Maji Zanzibar, walipofika katika ofisi za ZAWA Mabluu kuonana na Mkurugenzi kuhusiana na Mradi wa Jimbo la Kikwajuni la Uchimbaji wa Kisiwa na kusambaza maji katika jimbo hilo kuondoa kero hiyo, ukiwa katika hatua za mwisho za ufungaji wa Tangi Jipya katika Mnara wa Mbao Kilimani.  
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Masauni akizungumza katika mkutano huo na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Zaji Zanzibar, wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya maendeleo ya Jimbo lake  
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanibar Ndg Mustafa Ali Garu akizungumza katika mkutano huo wa kuzungumzia Mradi wa Maji katika Jimbo la Kikwajuni ambao uko katika hatua za mwisho kufungwa tangi la maji lililotolewa na Mbunge Mhe Masauni, baada ya kukamilika kwa uchimbaji wa Kisiwa katika hatua ya mwazo ya mradi huo. Utakaotosheleza kutowa huduma ya maji katika Jimbo la Kikwajuni.  

Mkurugenzi wa Taasisi ya The Registered Trustees of Communication for Development Africa Initiative, Ndg. Gaston Modest Kaziri, akizungumza katika mkutano huo na Mkurugenzi wa Maji Zanzibar, ikiwa Taasisi yake inayoshughulikia na utafutaji wa Wafadhili baada ya Wananchi kuibua miradi katika Majimbo yao.kushotoMbunge wa Kikwajuni Mhe Hamad Masauni.
Maofisa wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA wakifuatilia mkutano huo na Ujumbe wa Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe, Hamad Masauni. uliopofika ZAWA kwa mazungumzo.
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Hamad Masauni, akitowa maelezo kuhusiana na Kituo cha Vijana kinachotowa Mafunzo mbalimbali kwa Vijana wa Jimbo la Kikwajuni na majimbo mengi, Hutuoa Elimu ya Vijana Kujielewa, Ushauri Nasaha, Mafunzo ya Komputer na Vijana Kujiajiri wenyewe, ambacho kimeazishwa na Mhe Mbunge na kuwa Mlezi wa kituo hicho. wakati wa ziara ya kumtembeza Mgeni wake,  Mkurugenzi wa Taasisi ya The Registered Trustees of Communication for Development Africa Initiative, Ndg. Gaston Modest Kaziri, kujionea miradi ya Jimbo hilo ilioibuliwa na Mhe Masauni.
Mkurugenzi wa Taasisi ya The Registered Trustees of Communication for Development Africa Initiative, Ndg. Gaston Modest Kaziri, akizungumza na Vijana wa kituo cha Elimu kinchotowa Elimu kwa Vijana wa Jimbo la Kikwajuni, wakati wa ziara yake kutembelea miradi ilioibuliwa na Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni na Mbunge wao, kilichoko katika jengo la Wawi Muembemadema Unguja.  
Vijana wanaopata Elimu katika Kituo hicho cha TAYI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya The Registered Trustees of Communication for Development Africa Initiative, Ndg. Gaston Modest Kaziri,wakati wa ziara yake na Mbunge wa Kikwajuni.kujionea miradi ya Wananchi wa Jimbo hilo. 
Viongozi wa Kamati za Maendeleo katika Jimbo la Kikwajuni wakiwa katika ukumbi wa Mkutano katika kituo cha TAYI Muembemadema Unguja.
Vijana wanaopata Elimu katika Kituo hicho cha TAYI, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Taasisi ya The Registered Trustees of Communication for Development Africa Initiative, Ndg. Gaston Modest Kaziri,wakati wa ziara yake na Mbunge wa Kikwajuni.kujionea miradi ya Wananchi wa Jimbo hilo. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.