Habari za Punde

Vijana Walimu wa Madrasa na wa Vyama vya Siasa Zanzibar Washiriki Mafunzo ya Kupunguza Maambukizo ya UVV.

Afisa wa Miradi wa ZAYEDESA Ndg. Mgoli Lucians akitowa  maelezo ya  mafunzo hayo kabla ya kuaza  kwa Vijana washiriki wa mafunzo hayo kutoka Vyama vya Siasa Zanzibar na Waalim wa Madrasa Zanzibar, yalioandaliwa na UNESEF Tanzania kwa kushirikiana na Jumuiya ya ZAYEDESA, yaliofanyika katika Kituo cha Ushauri Nasaha miembeni Zayedesa Zanzibar. Ambacho hutowa huduma ya Bure kupima UVV. 
Mkufunzi wa Mafunzo ya siku moja kwa Vijana wa Vyama vya Siasa na Walimu wa Madrasa Zanzibar, Mahmoud Ibrahim akifafanua jinsi ya kupambana na kupunguza maambukizo ya Ukimwi kwa Vijana   

Washiriki wa mafunzo ya kupunguza maambukizo ya Ukimwi kwaVijana wakimsikiliza Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Mahmoud Mussa akitowa maelezo jinsi ya kujingia na maambukizo ya ukimwi kwa vijana.


Washiriki wa mafunzo ya kupunguza maambukizo ya Ukimwi kwaVijana wakimsikiliza Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Mahmoud Mussa akitowa maelezo jinsi ya kujingia na maambukizo ya ukimwi kwa vijana.
Mkufunzi wa Mafunzo kwa Vijana kuhusiana na maambukizo ya Ukimwi kwa Vijana Ndg Mahmoud Ibrahim  akisikiliza michango ya Washiriki wa mafunzo hayo. 
Mshiriki wa mafunzo hayo akitowa mchango wake na kuuliza swali kwa Mtoamaada kuhusiana na kinga ya kuzuia maambukizi.ya UVV 
Washiriki wa Mafunzo ya kupambana na kupunguza Maambukizo ya Ukimwi kwa Vijana Zanzibar akichangia mada katika mafunzo hayo yaliowashirikisha Viongozi wa Vyama vya Siasa, Walimu wa Madrasa Zanzibar,ilioandliwa na Jumuiya ya ZAYEDESA kwa kushirikiana na UNISEF Tanzania kutowa Elimu hiyo kwa Vijana, iliofanyika katika Kituo chaUshauri Nasaha cha ZAYEDESA miembeni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.