Habari za Punde

Karibu Zanzibar Makamu wa Rais wa China Mhe. Li.

Na Mwandishi wetu
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao, anaanza ziara ya siku mbili Zanzibar inayoanza leo.
Kiongozi huyo atawasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar saa 10:15 jioni  na kupokelewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.
Mhe.Yuanchao ambae atawasili nchini akitokea Dar  es Salaam, baada ya kufika atakwenda moja kwa moja Vuga kufanya mazungumzo na timu ya madaktari wa Kichina wanaotoa huduma katika hospitali za Zanzibar.
Baadae ataelekea Nungwi ambako atapata fursa ya kuzungumza na Balozi Seif , mazungumzo ambayo yatafanyika hoteli ya Lagema  na baadae kuhudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa na mwenyeji wake.
Kesho atatembelea mashamba ya viungo Kizimbani  na baade kutembelea Mji Mkongwe wa Zanzibar, ambako atatembelea Ngome Kongwe, Baitul- Ajab, soko la zamani la Watumwa na makumbusho.

Ujumbe wa kiongozi huyo utaondoka nchini saa 6:40 mchana ambapo ataagwa na Balozi Seif Ali Iddi.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Bwa.Li Yuanchao akiwa na Mwenyeki wake Makamu wa Pli wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakiangalia ngoma ya Utamaduni aina ya Msewe baada ya kuwasili Uwanja wa Ngede wa Kimataifa wa Abeids Amani Karume Zanzibar.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Bwa.Li Yuanchao , akisalimiana na Waziri wa Biashara Zanzibar Mhe Nassor Ahmeid Mazrui 



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao wakwanza kulia akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Zanzibar baada ya kuwasili,katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya watu wa China Li Yuanchao akisalimiana na Madaktari Mabingwa kutoka China wanaofanya Kazi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja alipowatembelea katika makazi yao Vuga Zanzibar..



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.