Habari za Punde

Mali kachara kudhibitiwa

Na Mwanajuma Mmanga
IDARA ya mazingira Zanzibar ipo mbioni kuandaa sheria ya kuwadhibiti wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa chakavu  kutoka nje.

Sheria hiyo inakuja baada ya kuonekana Zanzibar kuwa jaa la bidhaa chakavu kutoka ng’ambo ambazo huingizwa na wafanyabiashara au Wazanzibari wanaoishi nje ya nchi.

Mkurugenzi wa idara hiyo,Sheha Mjaja Juma, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofsini kwake Maruhubi.

Alisema Zanzibar sasa imekuwa jaa la bidhaa chakavu hali inayohatarisha mazingira na afya za wananchi.
Aidha alisema wakati mwingi bidhaa hizo huja sambamba na mende wengi wadogo, ambao wanasababisha athari kubwa katika makazi ya watu.


Alisema sheria hiyo iutasaidia kupunguza uingizaji wa bidhaa nyingi zisizokuwa na viwango.


Alitoa wito kwa wafanyabiashara kuingiza bidhaa zenye viwango badala ya kuingiza bidhaa chakavu kwa sababu tu wanazipata kwa bei rahisi au bure. 

5 comments:

  1. Tunaomba msicheleweshe hiyo sharia kwaajili ya kulinda nchi yetu kimazingira na kiafya. Inasikitisha tuliopo nje miaka yote hatuna cha kufikiria kujiendeleza kiuchumi na kuiwezesha nchi yetu kimaendeleo isipokuwa kuokota maused na kuyapeleka nyumbani,huu ni. Leo hii kila kona ya visiwa kuna mabki ya used yametelekezwa kutokana kutokuwa na recycle. Wenu Mkimbizi wa kiuchumi UK.

    ReplyDelete
  2. hali za maisha hapo kwetu kama munavyo ziona leo mtu alau anamiliki kiji fridge kibovu anapata maji baridi tena waheshimiwa munawaonea gere, na wewe Mkimbizi wa kiuchumi UK wewe hujawahi kupeleka used kwenu, au ndo Allah amekupa neema ndio unaanza kuleta kibri, kwakuwa wewe una uwezo wa kununulia wazee wako fridge jipya sio, sasa wale masikini za Mungu waendelee kudhalilika kwa maji yabaridi, mambo haya yanafanywa na nchi zilizoendelea kwasababu wao wanataka watu wanunue mafridge mepya kwasababu viwanda vitaendelea kuzalisha, wafanyakazi wataendelea kua na ajira, maduka yataendelea kukuwepo, wafanya kazi madukani wanaendelea na ajira zao huo ndio mzunguko, leo sisi wazanzibari tunafaidika nini tukipiga marufuku, hali za wananchi wanaweza kununua fridge jipya? au ndo muheshimiwa keshakatiwa chake na wafanya biashara.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ''na wewe Mkimbizi wa kiuchumi UK wewe hujawahi kupeleka used kwenu''. My friend Anonymous, electronic used ni hatari kwa afya ya binaadam na kimazingira pia. Ulitakiwa usisitize serikali ya SMZ ifunguwe recycle kwakuwa now dunia ni kijiji na Zbar kama sehemu ya dunia lazima itakuwa inaathirika katika maendeleo ya kiuchumi. Anyway ikiwa bidhaa mbovu au used ninavyojuwa mimi UK gov inavizuia visitoke ila mnatumia hilba kuvisafirisha. Unazani wazungu hawana akili wakwepe kukusanya kodi kwakukuzuieni musisafirishe mafriedge used? coz wanajuwa athari yake kwa afya ya binaadam. Don't take it personal

      Delete
  3. Hata mimi nakuunga mkono mchangiaji wa pili huyo wa mwanzo ni muongo wala hajui umaskini ni nini inaonekana yeye yupo kwenye wale wanaoiibiya serikali au wazee wake ni ccm maana ndio wanaouwezo wa kununua kitu kipya mshahara wa smz kwa mtu wa kawaida ni 180000 kwa mwezi sasa utalinunua fridi kwa milioni na nusu pole mchangiaji wa kwanza

    ReplyDelete
  4. Sheria ni msumeno hukeketa kila ncha.Idara ya Mazingira inaposema inaandaa sheria ya Zanzibar kutokuwa jaa ijuwe kuwa used ni used,sio fiji au friza tu lakini hata magari tunayopanda kama ni saloon au hata daladala yaingizwe katika orodha used. Maana yake ni kuwa sasa Zanzibar tutakuwa na vipya tuu maana hata yaho magari kwa lile wazo la kuingiza mnde linahusika. Lakini pia Idara ikumbuke ni makontena mangapi huingia kwa mwaka ikiwa ni ma-used jee yakiwa hayapo hasara ni kwa nchi gani na kwa serikali gani. Mimi naona kuwa Idara hii inajitambulisha kuwa imeshindwa na dhamana zake.Kama kushindwa kuwateketeza mende ni hija ya madai ya idara, naiuliza Idara nini maana ya fumigation na dhamana ya kuifanyia nchi au eneo fumigation ni dhamana ya nani jee wale mapanya na mabuku wanaletwa na mitumba? Tafuteni lakufanya na la kulitungia sheria,waacheni wanyonge wafanyabiashara watarazaki na walala hoi wanufaike.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.