Habari za Punde

Shirika la Huduma za afya la Marekani laonesha filamu katika Tamasha la Ziff

 Wananchi na waandaaji wa Filamu ya tohara kwa wanaume iliyotengenezwa na Lisa Russeli wakiangalia filamu hiyo katika Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree.
 Wananchi na waandaaji wa filamu ya Tohara kwa wanaume wakiangalia filamu hiyo hapo jana.
 
 Mkurugenzi wa Shirika la Huduma za Afya la Marekani (JHPIEGO) Nchini Tanzania Hally Mahler akielezea umuhimu wa tohara kwa wanaume na sababu zilizopelekea kufadhili na kuandaa filamu hiyo.
 Mkuu wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti maradhi ya ngono Dkt. Gissenge Lija akitoa maelezo ya Mpango huo baada ya maonyesho ya filamu ya umuhimu wa tohara kwa wanaume kwenye Tamasha la Kimataifa la Nchi za Jahazi (ZIFF).
 Msimulizi wa Filamu hiyo msanii Fareed Kubanda (Fid Q) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu madhara yanayowapata wanaume wasiofanyiwa  tohara hasa katika Mikoa ya Njombe  na Iringa Tanzania Bara.
Picha ya pamoja ya watengenezaji wa filamu ya umuhimu wa tohara kwa wanaume iliyowasilishwa kwenye Tamasha la Kimataifa la Nchi za Jahazi (ZIFF) katika Ukumbi wa Hoteli ya Double Tree Shangani Mjini Zanzibar.

 (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.