Na Fatma
Kassim, Maelezo
BODI ya
Chakula Dawa na Vipodozi, imeangamiza bidhaa chakula zenye uzito wa tani 25 baada
ya kubainika kuwa hazifai kwa matumizi ya binadamu.
Bidhaa hizo
ni pamoja na maziwa ya kopo aina ya NAN tani 7.4, soda za kopo, chama tani
tano, tende tani 10, mchele tani 1.1 na vyakula mchanganyiko tani moja ambapo
uangamizaji huo ulifanywa Kibele mkoa wa kusini Unguja.
Mkuu wa
ukaguzi wa bodi hiyo, Aisha Suleiman, alisema bidhaa hizo zimekamata kufuatia ukaguzi
unaofanywa bandarini, madukani na maghala yanayohifadhia bidhaa hizo.
Alisema soda
hizo zimeingizwa nchini zikiwa na tarehe iliyotengenezwa na hazina tarehe ya
kumala muda wa matumzi jambo ambalo linaweza kuhatarisha afya za watumiaji.
Alisema mchele
ulioangamizwa ni sehemu ya tani 26 za
mchele uliorejeshwa nchini Pakistan
baada ya kuonekana haufai kwa matumizi ya binaadamu.
Alisema
gharama zote za uangamizaji wa vyakula hivyo kwa mujibu wa sheria ya bodi,
zinatolewa na wenye mali .
Aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa bodi hiyo endapo
watatilia shaka bidhaa za aina yoyote ile zikiingizwa nchini au zikiwa madukani
kwa kuuzwa.
No comments:
Post a Comment