Habari za Punde

Waziri Zainab Awataka Watendaji wa Wizara yake kutumia Lugha Nzuri Wanapotowa Huduma.

Na Madina Issa
WAZIRI wa Ustawi wa Jamii, Vijana, Maendeleo na Watoto Zanzibar, Mhe. Zainab Mohammed Omar, amewataka wafanyakazi wa wizara yake kutumia lugha nzuri wakati wanapotoa huduma kwa jamii.
Alisema kutumia lugha chafu wakati wa kutoa huduma kunasababisha mvutano na wananchi na ni kitendo kisichokubalika.
Alisema hayo wakati akikabidhi vyeti kwa wafanyakazi bora wa wizara yake pamoja na kupongezana kwa kula chakula baada ya bajeti ya wizara hiyo kuidhinishwa na baraza la Wawakilishi.
Alisema wafanyakazi wana wajibu wa kuhakikisha wanawahudumia wananchi na kuwapa miongozo inayostahiki badala ya kuwadharau na kuwatolea lugha chafu.
Aliwahimiza wafanyakazi kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana ili kuiletea mabadiliko wizara hiyo.

Aliwapongeza wafanyakazi bora kwa kuchapa kazi na kuwahimiza kuongeza bidii ili kuiongezea ufanisi wizara hiyo na wao wenyewe.

1 comment:

  1. Mimi Jamani nataka kuuliza Huu Mtindo Wakupika NYALI na KUKU, MANYAMA na Kuwalisha ( ATI) Wafanyakazi Umeanzishwa na Nani?.. Na Nikwasababu Gani ?...

    Kwanini Waanzisher Mtindo huu baada ya Kupita kwa Badgeti zao ?... Hii Sio la Waziri Mmoja tu bali nimemshuhudia Mh. Sefu Ali Iddi akifanya Dhifa kjama hizi kila mwaka au mara kwa mara.... Hivo Ndio tuone kwamba Mawaziri Wanawapenda Wafanya kazi wao au ni kuharibu hela ya Walipa kodi tuu.....

    Kwanini Viongozi hawa Wasitoe Hela hiyo kwa mfumo wa Sadaka au zakka kwa wale wanaostahiki na badala yake hupika Nyali na Kuku wakawalisha Watu waliokua sio watendaji wazuri wa kazi zao.. Mawizara yote ya SMZ ina Wajuba Washenzi, na Watukanifu. Nashangaa jinsi ninavoona ubaguzi wa rangi, silka na hata pahala pa mtu anapotoka unavotendeka hapo katika wizara mbali mbali za SMZ...

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.