Na.Abdi Suleiman na Sada Ali, Pemba
HUDUMA za upasuaji katika hospitali ya
wilaya Chake Chake zimesitishwa kutokana na kuharibika mashine ya kuwawekea
dawa ya usingizi wagonjwa wanaohitaji
kufanyia upasuaji (anaesthetic machine).
Mashine hiyo iliharibika tokea Juni 20 mwaka
huu na kusababisha wagonjwa waliokuwa wamelazwa kusubiri kufanyiwa upasuaji
kuhamishiwa hospitali za Wete na Abdalla Mzee Mkoani.
Kuharibika kwa mashine hiyo ni pigo kwa
wagonjwa wanaofikishwa hospitalini hapo kufanyiwa upasuaji.
Baadhi ya madaktari, walisema mashine
hiyo iliyoharibika ni kongwe na ililetwa tokea mwaka 1992 wakati hospitali hiyo
ikianzishwa.
Aidha aliwasema mashine hiyo imeshafaniwa
matengenezo zaidi ya mara tano.
Akizungumzia suala hilo, Daktari bingwa
wa masuala ya upasuaji katika hospitali hiyo, Shaban Issa, alisema kuharibika
kwa kifaa hicho kumesababisha kuzorota kwa huduma za upasuaji.
Alisema tayari wameshaandika barua mara
kwa mara kuhusu ubovu wa mashine hiyo lakini bado juhudi za kutafutwa nyengine
hazijachukuliwa.
Alisema hospitali hiyo imekuwa ikifanya
upasuaji mkubwa kwa wagongwa kati ya watatu na wanne kwa wiki, mbali ya
wanawake wajawazito wanaozaa kwa upasaji.
Nae daktari dhamana wa hospitali hiyo,Yussuf
Hamad, alithibitisha kuharibika kwa mashine hiyo, huku akisema suala hilo liko kwenye mikono
ya Ofisa Mdhamini wa wizara hiyo.
Naye Ofisa Mdhamini wa Wizara ya Afya
Pemba, Dk. Mkasha Hija Mkasha, aliwataka wananchi kuwa na subra katika kipindi
hiki ambacho wizara inatafuta mbinu ya kupata mashine mpya.
SMZ CCM badala yakushuhulikia Huduma za Jamii kwa pesa ya Revenue.. Hela hiyo Hutiwa ndani ya Matumbo ya Viongozi wa SMZ ambao wengi wao Wanalipwa zaidi ya Millioni 4 kwa mwezi na kazi haijulikani..
ReplyDeletehapo sijataja Maraisi waliostaafu ambao Wanalipwa Millioni 2 kwa mwezi mbali marupu rupu ya Wafanyakazi na matibabu... Hao Viongozi waliostaafu Tukitizama hayo waliotuwachia hakuna hata moja la Maana labda Kuliwa kwa Wananchi na kugombanishwa wenyewe kwa wenyewe..
Hela nyengine Imeharibiwa kwakujengwa (ATI) Mnara wea Mapinduzi.. Pale Kisonge na Kuharibu Mazingira ya Mandhari ya Mji ule pamoja nakuzidisha Fitna inayotolewa na Walalahoi wa CCM katika maskani ya Kisonge...
Hela ile ingetumiwa kwa kuboreshwa Hospitali za Pemba, Library za mashule na mengineyo basi tungekua tumepiga hatua... Viongozi wa CUF waliomo Serikali Wanapopinga Sera za CCM zilizokua hazina Kipaumbele Wanaambiwa Wanataka Kuiua SUK na Ni Wasaliti wa Amani na Utulivu Zanzibar.... Hiyo Ndio SERIKALI YA CCM Iliojivisha jina la SUK na Ku-Hijacked Maridhiano ya Wazanzibari yaliokubaliwa na Mh. Amani Abedi Karume na Maalim Sefu Sharifu Hamadi....
Suk Imekua Hijacked na akina Sefu Ali Iddi na Sheni ambao hata kura Raisi wetui hakujipigia.. Alijiandikuisha Kwao Bara na kaletwa kua Raisi Zanzibar..