Na
Mwandishi wetu
KAMISHNA
wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai
Zanzibar (DCI), Salum Msangi, wamefunguliwa kesi mahakama kuu ya Zanzibar, baada
ya watu wanane waliokamatwa wakihusishwa na matukuo ya miripuko kuwekwa
kizuizini kwa muda mrefu bila kufikishwa mahakamani.
Kesi
hiyo namba 7 ya mwaka 2014 imepangwa kuanza kusikilizwa kesho mbele ya Jaji wa
mahakama kuu, Mkusa Issack Sepetu.
Washtakiwa
hao tayari wametakiwa kujibu hati za kiapo kabla ya kesi hiyo kuanza
kusikilizwa.
Kesi
hiyo imefunguliwa na Wakili Abdallah Juma Mohamed akishirikiana na Rajab
Abdallah Rajab kutoka kampuni ya uwakili ya AJM Solicitor ambao wanataka
mahakama kuwaita viongozi hao ili waeleze mahali walipo wateja wanane
wanaowatetea tangu walipokamatwa katika maeneo na nyakati tofauti visiwani
Zanzibar.
Kwa
mujibu wa hati hiyo ya kiapo, watu hao ambao wanadaiwa kukamatwa na kuwekwa
kizuizini ni Nassor Ahamad Abdallah, Mohamed Ishaq Yussuf, Said Kassim Ali,
Hassan Bakari Suleiman, Rashid Ali Nyange Antar Homuod, Khamis Salum Amour na
Salum Ali Salum.
Kesi
hiyo ya maombi ilianza kutajwa Ijumaa na Wakili Abdallah Juma Mohamed alidai walifungua
kesi hiyo kwa kuzingatia Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya
Zanzibar ambavyo zinaelezea haki ya washtakiwa.
Mkuu wa
Utawala wa jeshi la polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Aziz Juma Mohamed,
ambae alifika mahakamni kwa niaba ya Kamishna wa Polisi akiwa ameandamana na Naibu
Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Salum Msangi alisema wako tayari kusikilizwa kwa
ombi hilo.
No comments:
Post a Comment