Habari za Punde

Maalim Seif awafariji wagonjwa Mkoa wa Kusini Unguja






 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika ziara ya kutembelea na kuwafariji wagonjwa katika vijiji vya Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Na Hassan Hamad, OMKR
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo ameendelea na ziara yake ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa na wafiwa katika Mkoa wa Kusini Unguja.
 
Ziara hii ni mfululizo wa ziara zake za kuwatembelea wagonjwa katika maeneo mbali mbali Unguja na Pemba katika Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan, ambapo Alkhamis iliyopita alitembelea Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Akiwafariji wagonjwa hao, Mhe. Maalim Seif amewaombea wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kimaisha.
 
Nao wagonjwa hao wamemshukuru Makamu wa Kwanza wa Rais kwa kuamua kuwatembelea na kuwafariji, na kwamba ziara yake inaweza kuwa chachu ya kupata nafuu.
 
Katika ziara hiyo Maalim Seif ametembea wagonjwa katika vijiji mbali mbali vya Mkoa wa Kusini Unguja vikiwemo Kitogani, Kajengwa Makunduchi, Kibele na Umbuji.
 
Wakati huo huo Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Al-hajj Maalim Seif Sharif Hamad, jana alijumuika na Masheikh mbali mbali wa Zanzibar katika futari iliyofanyika nyumbani kwake Mbweni.
 
 
 

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.