Habari za Punde

Rais Kikwete awaongoza watanzania katika kuadhimisha siku ya mashujaa


Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kasimama kikakamavu wakati wimbo wa Taifa ukipigwa  kwenye Maadhimisho ya siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika bustani ya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo Julai 25, 2014
 
Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya mashujaa Tanzania zilizofanyika katika viwanja vya Manazi Mmoja Jijini Dar es salaam.
 
Rais Kikwete akijumuika takriban na Viongozi wakuu wote  wa Serikali zote mbili ile ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Ile ya Mapinduzi  ya Zanzibar wakiwemo pia wale wastaafu,Mabalozi wa Nchi rafiki waliopo Nchini, viongozi wa dini na wananachi wa kawaida aliweka Mkuki na Ngao kwenye Mnara wa kumbu kumbu za mashujaa sherehe ambazo hufanyika ifikapo tarehe 25 Julai ya kila mwaka.
 
Akisoma dua kwa upande wa madhehebu ya Dini ya Kiislamu kwenye maadhimisho hayo, mwakilishi wa dini hiyo sheikh Ali Muhidini alisema hii ni siku muhimu katika historia ya Tanzania hasa kwa kizazi cha sasa.
 
Sheikh Ali Muhidini alisema Watanzania wanapaswa kulazimika kuwa wazalendo wakati wote katika kutetea taifa lao hasa ile dhamira ya kupigania haki na uchumi wa Taifa.

Naye Baba Askofu wa Kanisa la CCT Steven Mang’ana  alisema Taifa la Tanzania linahitaji hali ya usalama, amani na upendo ile mola aendelee kuilea katika misingi hiyo muhimu.
 
Askofu Steven alimuomba Mwenyezi Muungu awaongoze njia iliyo sahihi wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba ili mjadala watakaoendelea nao mudfa mchache baadae uweze kuzaa katiba itakayoleta usawa na haki kwa jinsia zote.
 
Kwa upande wake Baba Lebaratus Libalio alisema kwamba Watanzania walio wengi hivi sasa wanaendele kufurahia amani na utulivu ulioasisiwa wa waasisi wa Taifa hili Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere na Mwenzake Marehemu Mzee Abeid Amani Karume.
 
Baba Liberetaus aliwataka na kuwahimiza Watanzania kuzidi kuwa na moyo wa upendo, mshikamano na maelewano miomngoni mwao sambamba na kuheshimu viongozi wanaowaongoza waliopo madarakani.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.