Na Mwashamba Juma, Beijing, China
WANAHABARI barani Afrika wametajwa
kuwa ni chachu ya kuibua na kuyatangaza mazuri yatokanayo na rasilimali na
maendeleo ya bara hilo kwa kutumia kalamu na kamera zao sambamba na kuonesha
uzoefu walionao kwa vyombo vya habari vya kimataifa ili kujenga uhusiano mwema
katika kuimarisha kada ya habari barani humo.
Hayo yalielezwa na Naibu Mhariri
Mtendaji wa gazeti la kila siku nchini China, “China Daily”, Gao Anming wakati
akifanya mazungumzo na ugeni wa maaofisa na wanahabari kutoka mataifa 12
yanayozungumza Kiingereza barani Afrika walipotembelea ofisi za kazeti hilo
mtaa wa Hu Xi, mjini Beijing.
Alisema ujio wa maofisa habari hao kwenye
ofisi za “China Daily ni mwema wa kufungua chaneli za urafiki baina yao katika kubadilishana uzoefu ikiangaliwa gazeti hilo tayari limefungua
milango na kuanza kusambaa kwa baadhi ya mataifa barani Afrika.
Alisema mbali na hatua kubwa
iliyofikiwa na “China Daily” ni mafanikio ya kusambaza gazeti hilo
karibu kila pembe ya dunia katika kuifikia hadhira yake, aidha aliongeza kuwa, kuweza
kufungua ofisi za kudumu na kuhakikisha gazeti hilo daima linasongambele na kukua
kibiashara.
“Mbali na mafanikio ya “China Daily” lenye
kurasa 26 lakini pia tunazalisha kopi za kila siku kwa “China Daily Hong Kong”
(1997), Marekani (2009), Amerika Kusini (2012), gazeti la wiki barani Ulaya “China
Daily European Weekly,” (2012), gazeti la kila wiki barani Asia (2010), Afrika
(2012) na Latin Amerika (2013) ambayo yote ni watoto wa “China Daily”
alifahamisha Naibu Mhariri huyo.
Alifahamisha barani Afrika “China
Daily” lina makao kuu yake mjini Nairobi , Kenya na tayari limefungua ofisi Tanzania kwa upande wa Afrika Mashariki na
kuongeza kuwa lengo la kuweka makao makuu ya gazeti hilo
Kenya ni kwamba kiingereza
kinazungumzwa sana nchini humo pia Nairobi , eneo lililobobea
kibiashara. Hata hivyo Gao alisema mwakani “China Daily” linatarajia kufungua
makao makuu yake nchini Misri na Nigeria .
Nae Mhariri Msaidizi wa China Daily,
Ji Tao wakati akitoa ufafanuzi kwa maofisa na wanahabari hao alisema gazeti lao
linajitahidi kuzalisha bidhaa zenye ubora kwenda sambamba na maendeleo ya
sayansi na teknolojia.
“Gazeti linajitahidi kuchapisha picha
zenye ubora na contenti ya hali ya juu katika kuyafikia malengo tuliyojiwekwea,
hii ni inatokana na ushindani wa teknolojia kwenye uzalishaji wa magazeti”
alifahamisha.
Abel Plackie Afisa habari, Mkurugenzi
masuala ya jamii, Wizara ya Habari Utamaduni na Utalii nchini Liberia, ambae
pia ni mkuu wa msafara wa maofisa na wanahabari hao alisema mwaliko wa China
Daily kwa wanahabari hao ni ishara na faraja njema katika kuunganisha nguvu moja
na kubadilishana uzoefu baina yao.
“Tunajisikia faraja na wenye bahati
kubwa kama wadau wa habari leo hii kuwa pamoja na wenyeji wetu, mbali ya kubadilishana
uzoefu nanyi, hatua mliofikia ni ya kupigiwa mfano, napenda pia kutumia fursa hii
kuishauri China Daily kuutumia ugenii huu kwa kuanzasha chaneli barani Afrika
ili kukidhi haja ya malengo yake kwa Afrika.” Alishauri mkuu huyo.
Sambamba na kulishauri gazeti hilo jenga uhusianao na mitandao ya jamii kama “Face book
na Twitta” katika kubadilishana mawazo na wanajamii kama moja ya vyanzo vya
habari, kwani kwenye jamii kuna mengi yakuibua kama
wanahabari.
“Mnaonaje mkatumia hii mitandaoo ya
jamii katika kupata taarifa na kuweka habari zenu kwani kunakojamii kuna mengi
na mnaweza kuibua mambo mengi. Alishauri.
Alisema “Chaina Daily” kusomwa dunia
nzima kwa ulimwengu wa sasa ni mafanikio makubwa hasa katika kuitangaza China
kwenye ulingo wa habari na uchumi dunuani kote.
No comments:
Post a Comment